Kufuatia kuongezwa
kwa kodi katika huduma za simu za mkononi , gharama za huduma hizo zinatajiwa
pia kuongezeka kuanzia Julai Mosi mwaka huu.
Taarifa ya pamoja
iliyotolewa jijini Dar es salaam na Umoja wa Makampuni ya Simu za Mkononi
Tanzania – MOAT imesema pendekezo la serikali la kuweka kodi ya 14.5 kwenye
huduma za simu za mkononi hazotoweza kukwepesha kupanda kwa gharama za simu kwa
watumiaji.
MOAT inasema awali kodi
ilikuwa ikitozwa asilimia 12.5 katika huduma ya mawasiliano ya simu na kwmaba
ongezeko la kufiikia asilimia 14.5 tofauti na nchi za jirani Kenya na Uganda
ambazo zimeendelea kutoza viwango vya ushuru vya asilimia 10 na 12.5 tu ni mzigo
kwa watumiaji wa huduma za simu za mkononi.
Muswada
wa Sheria ya Fedha wa mwaka 2013 unaainisha, huduma za mawasiliano kuwa ni;
“huduma yoyote ya maelezo inayotolewa na makampuni ya mawasiliano ya simu kwa
njia ya mawasiliano kwa kutoa au kupokea sauti, maandishi, na picha au taarifa
ya aina yoyote kupitia mfumo wa kielektronikia.
”Imesema taarifa hiyo
iliyosainiwa na Vodacom, Airtel, Tigo na Zantel MOAT imesema eneo mojawapo
litakaloathirika ni huduma za Intaneti eneo amablo linahitaji kuwekewa mikakati
ya kulikuza kutokana na umuhimu wake katika maisha ya sasa kiuchumi na kijamii
na wala sio kulizorotesha kwa kusababisha ongezeko la gharama na hivyo kuendelea
kuwa na kiwango cha cha matumizi kilinganishwa na baadhi ya nchi nyengine
zikiwemo za Afrika Mashariki.
“Hatua hii ya
kuongeza kodi itakwenda kinyume na mipango iliyopo yenye lengo la kuibadili
jamii kwa kuipatia maarifa ya msingi kupitia huduma ya intaneti sambamba na
mawasiliano ya simu.”
Kwa mujibu wa MOAT,
Tanzania ni kati ya nchi zenye kiwango cha chini ya matumizi ya huduma ya
mtandao wa intaneti katika bara la Afrika ambapo watumiaji wa huduma hiyo ni
asilimia 10 pekee ikilinganishwa na nchi jirani ya Kenya ambayo ina zaidi ya
watumiaji asilimia 40.
Aidha,
MOAT imeongeza kuwa, “mawasiliano ya simu si anasa bali ni huduma muhimu katika
Tanzania ya leo, sasa tunawezaaje kuwatozakodi mara kwa mara watu hao hao ambao
wanaitegemea huduma hiyo ili kuboresha maisha yao? Ilihoji taarifa hiyo ya
MOAT.
Taarifa hiyo
imeendelea kusema kuwa kwa tozo la kodi ya mapato ya asilimia 35 kwenye sekta
hiyo ya mawasiliano ya simu linatosha kiasi ya kwamba sekta hiyo isngeweza
kubeba mzigo zaidi wa ongezeko jingine.
Hivi sasa, upanuzi wa
mawasiliano na miundombinu vijijini ndiyo kipaumbele cha sekta nzima. Tunaamini
hapa ndipo ukuaji wa sekta ya mawasiliano ya simu itakapoonekana katika miaka
ijayo. Ongezeko lolote la kodi litazorotesha uwezo wetu wa kutanua huduma zetu
za mawasiliano na miundombinu maeneo ya vijijini, imesema MOAT.
“Tunaelewa kuwa serikali
inayafanya haya yote ili kuweza kupata fedha kwa ajili ya kusaidia kwenye huduma
za jamii katika maeneo muhimu. Ni bahati mbaya kwamba sekta ya huduma ya
mawasiliano ya simu inaendelea kubeba mzigo mkubwa wa ongezeko hili ambapo
wateja watalazimika kuelemewa na mzigo huo.
No comments:
Post a Comment