MKE wa naibu wa chifu 
katika wilaya ya Marigat Alhamisi aliaga dunia katika hali isioeleweka baada ya 
mumewe kumpata akinywa pombe haramu ya chang’aa katika nyumba ya 
jirani.
Naibu wa chifu wa kata ya Arabal Bw William Yegon inasemekana hakufurahia pale alipompata mkewe Bi Mary Kobilo, 46, akipiga mtindi na wanakijiji wengine.
Wenyeji walioongea na 
Taifa Leo walisema kuwa wawili hao walianza kuzozana wakati wa tukio hilo la saa 
kumi na mbili jioni Jumatano huku naibu huyo wa chifu akimlaumu mkewe kwa 
kumwaibisha kwa kunywa pombe hiyo haramu ilhali yeye alikuwa afisa wa serikali 
anayefaa kuongoza vita dhidi ya pombe 
haramu.
“Naibu huyo wa chifu alikasirishwa sana kwamba mkewe alikuwa akimkosea heshima licha ya serikali kutangaza vita kwa wapikaji wa pombe haramu,”alisema mmoja wa wanakijiji ambao hakutaka kutajwa jina.
Alisema kuwa baada ya ugomvi huo marehemu alipepesuka nje ya nyumba lakini hakwenda nyumbani kwake. Mwili wake ulipatikana katika msitu mmoja karibu na kwake Alhamisi mchana.Akithibitisha tukio hilo,mkuu wa wilaya ya Marigat Bw Saul Moywaywa alisema kuwa uchunguzi tayari umeanzishwa kubaini kiini cha kifo cha mwanamke huyo.Sumu“Mwili wake haukuwa na alama yoyote. Tunashuku alijitoa uhai wake kwa kumeza sumu,”Bw Moywaywa aliambia Taifa Leo kwa njia ya simu.Mwili wa marehemu ulichukuliwa na kupelekwa katika hifadhi ya maiti ya hospitali ya wilaya ya Kabarnet kusubiri upasuaji

No comments:
Post a Comment