Pages

Translate

Sunday, 23 June 2013


Lombero: Nazika Viungo Vyangu Nikiwa Hai


Maka Lombero
KWA mtu uliyekutana naye miaka saba iliyopita wakati huo akiwa dereva wa magari makubwa aliyefanya kazi zake mchana na usiku huku akilazimika kunyanyua baadhi ya mizigo mizito, si rahisi kuamini kuwa mtu huyo leo hawezi hata kufungua mlango wa gari.
Huyo si mwingine bali ni Maka Lombero (39) mzaliwa wa Bukoba, mkazi wa jijini Dar es Salaam ambaye anaishi maisha duni baada ya kukumbana na masahibu yaliyosababisha kukatwa kiungo kimoja baada ya kingine na kumwacha akiwa hana viganja vya mikono yote miwili na mguu wa kushoto.
Nilikutana na Lombero saa mbili na nusu usiku eneo la Kigogo Luhanga akiwa amekaa nje ya duka, huku ameengemea fimbo yake ya kutembelea. Nilipomsalimia alionekana ni mtu mwenye furaha asiye na wasiwasi wowote. Aliinua mkono wake uliokatika nusu na kuuelekeza kwangu akitaka nimsalimu kwa kumpa mkono.
Nilimpa mkono naye kwa furaha akaniambia: “Karibu ndugu yangu.” Huku akisogea niweze kukaa lakini kwa kuwa nafasi ilikuwa ndogo nilimwomba tuingie katika mgahawa uliokuwa karibu ili kuweze kuzungumza. Alichukua magongo yake ya kutembelea, kisha taratibu tukaingia ndani.
Alipoanza kunisimulia historia ya maisha yake ghafla furaha aliyokuwa nayo ilitoweka huku machozi yakimlenga. Kwa kuwa nilihitaji sana kujua historia ya maisha yake nilibadilisha mada kwa kumuuliza angependa kula chakula gani.
“Mimi situmii mayai, kama kuna viazi (chipsi) na mishikaki itanitosha,” alisema Lombero.
Wakati tukisubiri chakula alinieleza namna anavyokula; “Ndugu yangu, nina kula kama mbwa au paka. Ninaweka mdomo wangu kwenye sahani ya chakula na kuanza kula. Ni mateso tu niliyonayo,” anasema.
Anadokeza kuwa anahisi matatizo ya kuoza kwa viungo kulikosababisha akatwe mikono na mguu kunatokana na vitendo vya kishirikina alivyofanyiwa, baada ya kumpiga msichana mmoja ambaye aligombana naye katika mtaa wa TRM barabara ya Dodoma, Iringa mjini. “Kuna msichana tulipishana kidogo kauli akanipiga na tofali mgongoni, nilimpiga sana siku chache baadaye matatizo yalianza,” alifafanua.
Historia yake
Lombero anasema kuwa alihitimu elimu yake ya msingi mwaka 1988 huko Bukoba. Mwaka 1990 alijiunga na shule ya sekondari ya Mnazi Mmoja ya Jijini Dar es Salaam, aliposoma kwa miaka miwili na kuamua kuacha masomo kisha kwenda Tunduru kuchimba madini ya vito.
Mwaka 1995 familia yake ilimpeleka Morogoro kwenda kujiunga na Chuo cha Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) kilichopo Kihonda, ambako alifanikiwa kupata leseni ya kuendesha magari makubwa. Baada ya kuhitimu masomo alikaa mtaani kwa siku chache kabla ya kwenda Ifakara kwa baba yake ambako alipata kazi ya kuendesha lori katika kampuni ya Zaniri.
“Ile kampuni nilikaa nayo muda mfupi tu baadaye nilikuja Dar es Salaam nikapata kazi kwenye kampuni ya Mwarabu,” anasema na kuongeza kuwa kampuni hiyo alifanya nayo kazi muda mrefu ikilinganishwa na ile ya kwanza.
Baada ya kuacha kazi alikwenda Zanzibar kufanya kazi katika kampuni ya Zanzibar Cable, aliyodumu nayo kwa mwaka mmoja tu. Akiwa huko alifunga ndoa na Salima Lukas aliyezaa naye watoto wawili; mmoja wa kiume na mmoja wa kike.
“Tulipotoka Zanzibar, mwaka 2007 tulikwenda Iringa kwa wazazi wa mke wangu, tukiwa huko tukaanza biashara ya kuuza mkaa na huko ndiko ugonjwa ulipoanza,” alisema Lombero.
Matatizo yalivyoanza
“Nakumbuka ilikuwa ni saa tisa usiku nikiwa nimelala ndani ya kibanda kidogo cha udongo msituni tulikokuwa tunachoma mkaa, ghafla usingizi uliisha nikawa nahisi kuna watu wananipuliza, nilijaribu kuinuka lakini sikufanikiwa,” ndivyo anavyoanza kusimulia mkasa wake.
Anasema wakati akiendelea kutafakari kitu gani kinamtokea, ghafla kidole chake cha shahada (Ni kidole cha pili kutoka kidole gumba) cha kulia kilianza kuuma kama vile kuna mtu alimkanyaga.
“Nilipoangalia pembeni niliwaona watu watatu wamevaa ushungi wamesimama pembeni yangu sikuweza kuwatambua. Baadaye wale watu walitoweka.” Aliongeza.
Kuna mtu mmoja ambaye alikuwa akipita na baiskeli kila siku asubuhi na kumsalimia, huyo ndiye aliyemsaidia kumpa huduma ya kwanza kisha akampeleka kwa mganga wa kienyeji anayefanya kazi zake Ilula wilayani Kilolo.
“Mganga aliniambia kuwa kiganja changu kina chale tatu ambazo wakati wote huo nilikuwa sijaziona,” anasema na kuongeza kuwa: “Kwa kuwa nilikuwa na maumivu makali nilimsaidia kuziweka dawa kwenye chungu na kusogeza kuni kwenye moto ili anihudumie haraka maumivu yaishe.”
Baada ya dawa kuchemka kwa muda mrefu aliziweka juu ya mkono wake na kumwambia, kama atasikia maumivu yanakuwa makali zaidi asema ili waitoe dawa hiyo. Kitu cha ajabu kilitokeo alipotoa zile dawa mkononi, ndani ya zile chale tatu vilitoka vipande vitatu vya vioo; viwili vya kijani na kimoja cheupe. Akamwambia aende nyumbani lakini arudi siku ya pili.
“Nilipofika home (nyumbani) nilikuwa mzima kabisa, nikamsimulia wife (mke) kusudi aamini ninachomwambia nikapiga ‘pushapu’ kadhaa, sikusikia maumivu kabisa,” alieleza.
Siku ya pili alipokwenda kwa mganga alipewa dawa, kama ilivyokuwa siku ya kwanza kitu kingine kikatoka katika zile chale, wakati huu kikatoka kipande cha mkaa. “Akaniambia niende tena siku ya tatu kwa sababu kuna kitu kibishi kinagoma kutoka,” aliongeza.
Alisema akiwa kwa mganga, huku nyuma mke wake alimpigia simu mama mzazi wa mume wake akimtaarifu hali aliyonayo mwanawe. Mama mzazi na mkewe walimzuia kurudi kwa mganga kwa madai kuwa anatapeliwa.
Maumivu kwenye kidole yalirudi kama yalivyokuwa mwanzo huku kidole kikibadilika rangi na kuanza kuwa cheusi. Asubuhi iliyofuata alipandishwa kwenye basi kuelekea Dar es Salaam kwa ajili ya matibabu.
Alipofika Dar es Salaam alipelekwa hospitali ya Kairuki kufanyiwa uchunguzi ambapo ilibainika kuwa mishipa inayopitisha damu kwenye kidole

No comments:

Post a Comment