Pages

Translate

Sunday 23 June 2013

HENRY KILEWO ANASHIKILIWA NAPOLISI KWA SIKU YA 3 LEO HUKU MKEWE HAJUI ALIKO


                                 Henry Kilewo na mkewe
KAIMU Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mkoa wa  Dar es Salaam, Henry Kilewo, anashikiliwa  na polisi kwa siku ya tatu leo, akihusishwa na  tukio la kumwagiwa tindikali, Musa Tesha.
Tesha alimwagiwa tindikali na watu wasiojulikana Septemba 9, mwaka juzi kwenye kampeni ya uchaguzi mdogo wa Jimbo la Igunga, uliomuweka madarakani Dk. Kafumu Dalali.
Akizungumza juzi na Tanzania Daima kabla ya kufika makao makuu ya Jeshi la Polisi, Kilewo alisema hajui anachoitiwa na kwamba anatekeleza wito wa jeshi hilo kuwa afike ofisini kwao.
“Sijui ninachoitiwa, nimepigiwa simu naenda kutekeleza wito, nimesha wataarifu mawakili wangu ninaowaamini, kwa kuwa chochote kinaweza kutokea cha msingi Watanzania wapenda mageuzi waniombee kwa Mungu,” alisema Kilewo.

Wakili wa Kilewo, Peter Kibatala, alisema baada ya mteja wake kuhojiwa kwa muda wa saa tano juzi alielezwa kuwa anapelekwa Igunga, mkoani Tabora kuunganishwa na watuhumiwa wengine katika kesi ya kutumia tindikali na kujeruhi.
Kibatala alisema anasikitishwa na hatua ya jeshi hilo kumnyima dhamana mteja wake ilhali kosa wanalomtuhumu linadhaminika na kwamba hayo ni matumizi mabaya ya madaraka kumzuia mtu kwa zaidi ya saa 24 pasipo kumfikisha mahakamani.
Wengine wanaoshikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kutumia tindikali na kudhuru watu ni pamoja na  Oscar Kaijage wa Shinyanga na Evodius Justinian wa Bukoba.
Evodius Justinian alikamatwa na  Jeshi la Polisi mjini Bukoba na kushikiliwa kwa siku kadhaa kabla ya  kusafirishwa hadi jijini Dar es Salaam.
Kabla ya kusafirishwa na kufikishwa jijini Da r es Salaam, Justinian alieleza kuteswa na kupigwa na askari waliokuwa wakimzuia katika vituo mbalimbali kuanzia mjini Bukoba.

Wakati haya yote yakitokea nae mkewe amtuma njiwa kupeleka salamu kwa mumewe


Joyce Kiria....Ameandika hivi katika ukurasa wake wa Facebook
"Nimempelekea Henry chakula cha jioni majira ya saa 11 jioni hii pale central police, nikaambiwa wameshamchukuwa! Nikauliza kaenda wapi askari wa mapokezi akaniambia hata yeye hajui! Nikacheki na wakili Kibatala akaniambia hata yeye hana taarifa kama wamemchukuwa! Wapi haki ya mtuhumiwa? Familia yake haipaswi kujua anaenda wapi? Hata wakili anafichwa? Am so confused...

Ee Mungu mpiganie Mume wangu Henry popote alipo. Usimwache ahuzunike hata kidogo bali umpe nguvu ktk kipindi hiki cha mpito. Amen

My sweetheart Henry be strong, hata kama sipo na wewe physical lkn nipo pamoja na wewe mpz wangu. Mungu ni mwaminifu atatushindia.. Lv you big time mwaaaaa

Njiwa peleka salam
" Joyce Kiria


 

No comments:

Post a Comment