Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Moh’d
Shein amewataka wananchi wa Mangapwani kulinda, kuenzi na
kuendeleza Utamaduni wa asili wa Zanzibar ili kuweka historia kwa
kizazi cha baadae.
Dk. Shein ameyase mahayo leo huko Mangapwani Mkoa wa Kaskazini Wilaya
ya kaskazini B Unguja, wakati alipokuwa akizinduwa Tamasha la Urithi
la wana kijiji cha Mangapwani linalohamasisha kuinua hali za maisha
ya kijiji na kutunza historia ya kijiji hicho.
Amesema historia ni kitu muhimu sana kwa mwanadamu kufahamu yale
yaliopita ambayo yalikuwa muhimu na kutoa mchango mkubwa kwa wana
kijiji hivyo kuitunza historia ya watu wa Mangapwani ni jambo muhimu kwao
na Taifa kwani litapelekea kupata kipato kutokana na wageni (watalii )
wanaoingia kijijini hapo .
“Mambo ya asili yasitupwe yaendelezwe, leo vijana wanapoteza muelekeo kwa
kusahau ya zamamani walio kuwa wakiyafanya wazee ambayo yaliwaongezea
afya kujenga miili yao kwa kula vya kula vya asili lakini leo chipsi
zimetawala na vijana kuwa na matatizo ya kiafya kwa kula mafuta kuzidi
kipimo.” alisema Dkt Ali Mohamed Shein.
Aidha Dkt. Shein alisema njia nzuri ya kuutunza na kuendeleza
utamaduni ni kutunga vitabu na kuviuza vitakavyoelezea Historia,
Tamaduni na Silka za kijiji hicho ili wakija wageni kutoka nchi
mbalimbali wavikute na kujisomea.
Aidha Rais wa Zanzibar na Mwenyeki wa Baraza la Mapindunzi Dkt Ali
Muhamed Shein alisema kua matamasha kama hayo ni mazuri na ni muhimu
sana kufanyika katika maeneo ya historia kwani hueleza hali halisi ya
sehemu kama hizo ambazo zilikaliwa na wakoloni kwa kufanya shughulizao
mbalimbali kama vile ulinzi na usalama.
“ Ngome sehemu ya Mangapwani ilitumika katika masuala kama vile ulinzi
na usalama kwa kujenga ghala la silaha ili kujilinda na
maaduwi”alisema Dkt Shein.
Hata hivyo Dkt Shein alimpongeza Rais mstaafu Mzee Ali Hsani Mwinyi
kuwa mlezi wa tamasha hilo na kusema kua anamshukuru kwa ujasiri wake kukubali kuwa mstari wa mbele na kuona tamasha hilo linafanikiwa .
Akijibu risala ya wana kijiji wa hapo juu ya kupatiwa eneo la ujenzi
wa chuo cha uvuvi na utengenezaji wa magari alisema jambo hilo ni zuri
na atamuagiza Waziri wa Ardhi Ramadhali Abdalla Shabani kuangalia
uwezekano wa kuwapatia wana kijijihicho eneo la kutimiza azma yao .
Nae Rais Mstahafu Ali Hassani Mwinyi alisema kuwa kuna haja ya kurejesha
hadhi ya Mangapwani pamoja na mambo ya asili ambayo yamepotea kwa
siku nyingi . Amesema mangapwani ya zamani si ile yaleo ambayo vivutio vyake vina potea jambo ambalo kuna haja kubwa kutunzwa na wannchi kufaidika navyo.
"Irudishwe hadhi ya mangapwani kwani mcheza kwao hutuzwa,” alisema Mzee Ali.
Aidha alisema kua tamasha hilo ni kutafuta nia ya kuwawezesha
wanakijiji wa ukunda huo wa mangapwani na jirani zao kuwawezesha
kiutalii na utamaduni pamoja na kuwakumbuka wasanii marufu wataarabu
hapa Zanzibar.
Nae mwenyekiti wa Tamasha hilo Mwinyi Jamal Nasib akisoma Risala
kwa niaba ya wanakijiji cha mangapwani kwenyetamasha hilo alisema
malengo makuu ya Tamasha ni kurejesha utamaduni ulio potea
,asilizawatu wa hapo,kutafuta dawa ya kujikwamua na umasikini,
kuendeleza utalii na kujenga chuo cha kumuenzi Rais Mstaafu Mzee Ali
Hssan Mwinyi ambae ni mlenzi wa Chuo hicho.
IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR
No comments:
Post a Comment