Pages

Translate

Saturday, 15 June 2013

DK EMMANUEL NCHIMBI AFUNGA MAFUNZO YA UONGOZI NGAZI YA JUU KWA MAAFISA WA MAGEREZA UKONGA, DAR ES SALAAM LEO



Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi akikagua gwaride la wahitimu kozi namba 20 ya mwaka 2013 ya Uongozi ngazi za juu kwa maafisa wa Magereza. Sherehe hizo zimefanyika katika chuo cha maafisa magereza Ukonga, jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi akimvisha cheo cha Mrakibu Msaidizi wa Magereza, Hamza Abdalla kwa niaba ya wahitimu wa kozi namba 20 ya mwaka 2013 ya Uongozi ngazi za juu kwa maafisa. Sherehe hizo zimefanyika katika chuo cha maafisa magereza Ukonga, jijini Dar es Salaam.
Gwaride la wahitimu kozi namba 20 ya mwaka 2013 ya Uongozi wa ngazi za juu kwa maafisa wa magereza likipita kwa mwendo wa haraka mbele ya mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi (hayupo pichani). Dk Nchimbi aliyafunga mafunzo hayo katika chuo cha maafisa wa magereza Ukonga, jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi akizungumza na askari na maafisa magereza kabla ya kufunga mafunzo ya Uongozi wa ngazi za juu kwa maafisa wa magereza kozi namba 20 ya mwaka 2013. Sherehe hiyo ilifanyika katika Chuo cha Maafisa wa Magereza Ukonga, jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment