Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari kutoka Tanzania bara na Zanzibar walipata fursa ya kutembelea wadau mbalimbali wa kilimo wakiwemo wakulima wenyewe ilikujionea hali halisi katika sekta hii nchini. Waandishi hao ambao walipata fursa hiyo chini ya bioscience for farming in Africa nchini ( B4FA) walitembelea wakulima, watafiti wa mbegu, tissue cultures pamoja na wakaguzi wa mimea nchini. Fursa hiyo ilitolewa ili kuruhusu waandishi wa habari kujionea uhalisia wa mambo na kujipanga upya kutoa elimu kwa wananchi juu ya kilimo bora kinachoendana na zama hizi za digital katika kutumia sayansi na teknolojia ili kujikwamua kiuchumi. Kama ijulikanavyo kuwa kilimo ndio uti wa mgongo wa Tanzania bado sekta hii imeachwa nyuma na msemo huo kubaki vitabuni na si kiuhalisia. Pamoja na jitihada za serikali kujikita katika kilimo kwanza pia zana hii imebaki kuwa maneno na si kimaendo kwakuwa mkulima wa Tanzania hajui nini manufaa ya kilimo kwanza. Hata hivyo kilimo cha Tanzania bado kina changamoto nyingi ikiwemo kuwepo kwa mbolea feki, mbegu feki, ukame, pamoja na ushirika mdogo kati ya wataalam na wakulima. Mambo ambayo yanatakiwa kutiliwa mkazo kama kweli kilimo ni uti wa mgongo wa Tanzania ni kuanzia uwekezaji katika uzalishaji wa mbegu bora kazi ambayo AVRDC ya mkoani Arusha wanaifanya kama ambavyo waandishi walijionea mkoani Arusha
Mahali maalum kwa ajili ya uoteshaji wa mbogamboga AVDRC
Aina tofauti tofauti za mboga mboga zikiwa shambani
Baadhi ya Mbegu zikiwa zimehifadhiwa kiusalama kabisa katika chupa maalum kwa kazi hiyo AVRDC
Waandishi wa habari wakimuhoji Bwana Hassan Mndiga kuhusiana na utaalam wake kuhusu mbegu wanazozalisha.
kilimo bila kushirikiana na wataalamu ni kazi bure kwani ni sawa na kipofu kumwongoza kipofu mwenzie. msemo huu niufananisha na jinsi ambavyo wakulima wamekuwa wakifanya kazi zao bila kupata mwongozo kutoka kwa wataalam. Ili mkulima aweze kufanikiwa nilazima mbegu anazozitumia ziwe bora, mvua za kutosha pamoja na kufuata kanuni zote za kilimo.AVRDC ni wazalishaji na watafiti wa mbegu mbalimbali kwa ajili ya matumizi kwa wakulima. kiwanda hiki kimekuwa mstali wa mbele kufanya utafiti wa mbegu bora kulingana na mazingira husika. Lakini imekuwa ni kazi ngumu kwa mbegu hizi kuwafikia wakulima kutokana kwamba wao huzalisha na kufanya utafiti na kuwapa wauzaji ili kuzifikisha kwa wakulima, lakini kwa bahati mbaya sana wakulima huzipata mbegu hizi kwa kuchelewa na wakati mwingine hupata mbegu feki kutokana nachangamoto mbali mbali zilizopo katika sekta ya kilimo. Serikali yatakiwa ujipanga ili kumwinua mkulima kwani mara zote tumekuwa tukisema kuwa kilimo ni uti wa mgongo wa Tanzania lakini bado sekta hii imeachwa nyuma. Viwanda kama AVDRC vipo nchini mwetu lakini ni wakulima wachache sana wanaojua uwepo wa viwanda hivi na wakati mwingine watu hutumia nembo yao kuuzia mbegu feki kwa wakulima wakati wao si wauzaji bali ni wazalishaji na watafiti. AVDRC wamekuwa mstari wa mbele kuzalisha mbegu zinazostahimili hali ya hewa ya mahali husika.
Mkulima Allan akiwa shambani kwake
Imekuwa ni dhana ya watu wengi kuona kilimo hakina manufaa baada ya kuona nguvu nyingi hutumika katika kilimo lakini mafanikio ni madoga tena yasio na tija kwa wakulima na kubaki akiwa ndio wenye kipato duni nchini. Dhana hiyo ambayo Bwana Allan anaiona ni kinyume mara baada ya yeye kugundua siri ya kufanya kazi ya kilimo kwa kufuata ushauri kutoka kwa wataalam. Allan ambaye ni Mmeru, mkulima na mkazi wa tengeru wilayani Meru Mkoani arusha amekuwa mfano wa kuigwa kwa majirani na marafiki kwakuwa yeye amepata manufaa makubwa kupitia kilimo. kitu ambacho kimemsaidia kubadili maisha yake kiujumla kwani amekuwa akilima mara tatu kwa msimu kwa kutumia begu zilizoboresha (hybrid) na kulima kwa kubadili mazao shambani {crop rotation}ili kuepusha mazao kushambuliwa na magonjwa kitu ambacha anadai kutokukifanya hapo awali kabla hajakutana na wataalamu wa kilimo kwa ushauri. Pia bwana Allana ameomba wataalamu wa kilimo kufanya kazi bega kwa bega na wakulima kwani uwezekano wa kubadili hali ya mkulima wa chini kutoka katika hali duni na kufika juu zaidi inawezekana endapo kama watakuwa ni wataalamu wa vitendo na si maneno kama siasa.
mbegu za migomba zikiwa bado zipo katika kifaa maalum kwa kuzalishia mbegu hizo
watanzania inabidi tuondokane na mtazamo duni wa kuongea na kupanga sana bila kuwa na utekelezaji vitu ambavyo ni ugonjwa mkubwa nchini. Msemo huu unakuja kutoka na kwamba wataalamu wengi wapo sana maofisini wakitoa maagizo bila ya kuwa mstali wa mbele katika utekelezaji. Viongozi wa serikali inabidi kuondokana na mtazamo wa kimazoea na kubadirika ili kufanya kazi zenye tija kwa jamii haswa katika sekta muhimu kama kilimo. Wapo mawaziri ambao hawajawahi hata siku moja kuwatembelea wakulima na kuwauliza matatizo yao kitu ambacho hakifai kabisa kutokea. Wapo wataalam na wakulima amboa wanatamani sana kama wangepewa nafasi ya kukutana na waziri wakilimo ili tu aseme nae neon lakini hawana nafasi hiyo. Viwanda kama TBL badala ya kudhamini burudani na mpira isisahau kuwa ngano na shairi ni mazao wanayoyatumia kuzalishia vinywaji, hivyo ni wajibu wao pia kudhamini tafiti za begu bora za mazao haya ili kuepukana na ghalama za kununua mazao hayo kutoka nje na badala yake wakulima wa ndani watalima na kuwanufaisha wao pia. hivyo basi ipo sababu ya kutazama na upande wa pili ili kuona nini chakufanya katika udamini. Wapo vijana ambao wanatamani kama wangelikuwa na pakuanzia na kufanya kitu kinachoonekana katika jamii lakini hawajui wapi wataanzia, lakini kumbe wakidhaminiwa wanaweza kuondokana na wimbi la mabaya ambalo linamaliza vijana amboa ndio nguvu kazi ya taifa letu
Mahali maalum kwa ajili ya uoteshaji wa mbogamboga AVDRC
Shamba la aina za michicha mabalimbali maalumu kwa kuzalisha mbegu za mchicha
Aina tofauti za mbegu zikiwa kwenye hatua za ukaushaji
Aina tofauti tofauti za mboga mboga zikiwa shambani
Dr Tsvelina Stoilovna akitoa maelezo jinsi ya kuhifadhi gene.
Baadhi ya Mbegu zikiwa zimehifadhiwa kiusalama kabisa katika chupa maalum kwa kazi hiyo AVRDC
Waandishi wa habari wakimuhoji Bwana Hassan Mndiga kuhusiana na utaalam wake kuhusu mbegu wanazozalisha.
kilimo bila kushirikiana na wataalamu ni kazi bure kwani ni sawa na kipofu kumwongoza kipofu mwenzie. msemo huu niufananisha na jinsi ambavyo wakulima wamekuwa wakifanya kazi zao bila kupata mwongozo kutoka kwa wataalam. Ili mkulima aweze kufanikiwa nilazima mbegu anazozitumia ziwe bora, mvua za kutosha pamoja na kufuata kanuni zote za kilimo.AVRDC ni wazalishaji na watafiti wa mbegu mbalimbali kwa ajili ya matumizi kwa wakulima. kiwanda hiki kimekuwa mstali wa mbele kufanya utafiti wa mbegu bora kulingana na mazingira husika. Lakini imekuwa ni kazi ngumu kwa mbegu hizi kuwafikia wakulima kutokana kwamba wao huzalisha na kufanya utafiti na kuwapa wauzaji ili kuzifikisha kwa wakulima, lakini kwa bahati mbaya sana wakulima huzipata mbegu hizi kwa kuchelewa na wakati mwingine hupata mbegu feki kutokana nachangamoto mbali mbali zilizopo katika sekta ya kilimo. Serikali yatakiwa ujipanga ili kumwinua mkulima kwani mara zote tumekuwa tukisema kuwa kilimo ni uti wa mgongo wa Tanzania lakini bado sekta hii imeachwa nyuma. Viwanda kama AVDRC vipo nchini mwetu lakini ni wakulima wachache sana wanaojua uwepo wa viwanda hivi na wakati mwingine watu hutumia nembo yao kuuzia mbegu feki kwa wakulima wakati wao si wauzaji bali ni wazalishaji na watafiti. AVDRC wamekuwa mstari wa mbele kuzalisha mbegu zinazostahimili hali ya hewa ya mahali husika.
Mkulima Allan akiwa shambani kwake
Imekuwa ni dhana ya watu wengi kuona kilimo hakina manufaa baada ya kuona nguvu nyingi hutumika katika kilimo lakini mafanikio ni madoga tena yasio na tija kwa wakulima na kubaki akiwa ndio wenye kipato duni nchini. Dhana hiyo ambayo Bwana Allan anaiona ni kinyume mara baada ya yeye kugundua siri ya kufanya kazi ya kilimo kwa kufuata ushauri kutoka kwa wataalam. Allan ambaye ni Mmeru, mkulima na mkazi wa tengeru wilayani Meru Mkoani arusha amekuwa mfano wa kuigwa kwa majirani na marafiki kwakuwa yeye amepata manufaa makubwa kupitia kilimo. kitu ambacho kimemsaidia kubadili maisha yake kiujumla kwani amekuwa akilima mara tatu kwa msimu kwa kutumia begu zilizoboresha (hybrid) na kulima kwa kubadili mazao shambani {crop rotation}ili kuepusha mazao kushambuliwa na magonjwa kitu ambacha anadai kutokukifanya hapo awali kabla hajakutana na wataalamu wa kilimo kwa ushauri. Pia bwana Allana ameomba wataalamu wa kilimo kufanya kazi bega kwa bega na wakulima kwani uwezekano wa kubadili hali ya mkulima wa chini kutoka katika hali duni na kufika juu zaidi inawezekana endapo kama watakuwa ni wataalamu wa vitendo na si maneno kama siasa.
Bwana Allan (wa kwanza kulia) akiwa na wenzake shambani kwake
Shamba la mahindi la Bwana Allan
Mbali na bwana Allan pia Bi Hellen George wa kijiji cha Engorore, Kisongo Mkoani Arusha alitoa siri ya kubadili mfumo wa maisha yake kutoka kwenye mkulima asiye na kitu mpaka kuwa mfano wa kuigwa kijijini kama sio na wanakikundi wenzake kutokana na kupata mafanikio makubwa kutokana na kufuata kanuni na hatua za kilimo bora. Pamoja na mji wa Kisongo kukumbwa na ukame kwa kipindi cha msimu wa kilimo kilichopita lakini Bi Helleni amefanikiwa kupata mavuno kutokana na kutumia mfumo wa kulima hahindi yakiwa yamechanganywa na mazao yakufunika udongo ili kuzuia upotevu wa maji toka ardhini(cover crop) mazao hayo ambayo ametumia kufunika udongo ni pamoja na ngwara, kunde na maharage ambayo yote ni faida kwa ke kwa wakati mmoja. Mbinu hii ambaya aliipata kutoka kwa NGO's ya RECODA ambayo ipo mjini arusha na kazi yake ni kuwainia wakulima kwa kuwafundisha mbinu za kilimo bora na jinsi ya kukabiliana na umaskini kutokana na kilimo. Yeye pia ni mfugaji wa mbuzi na kuku wa kienyeji lakini kwa kutumia mfumo wa kisasa ambao ni faida kwake kwani ameondokana na dhana ya yeye na mifugo kwenda kazini na kurudi wote wakiwa wamechoka na mwisho wake kutopata kitu.
Bi Hellen akiwahudumia mbuzi wake wa maziwa
Banda la kuku la Bi Hellen
Bi Hellen akiwa shambani kwake na kiongozi wa B4FA bi Claudia Fichtner
Mbegu za ngwara zao analolima Bi Hellen maalum kwa biashara
Shamba la migomba ambayo ni moja ya matunda yanayompatia kipato pia ni chakula kwa mbuzi wake Bi Hellen
Shamba la mahindi likiwa linamchanganyiko wa mazao mengine kama ngwara kunde kwa ajili ya kufunika udongo usipoteze maji kutokana na ukame
Wakulima wadogo wadogo kama Allana na Hellen ni mfano wa kuigwa na tutafika mbali kama elimu zaidi itatolewa kwa jamii nzima ili kukomboa nchi yetu kutoka kwenye janga la njaa. Kilimo kwanza isiwe ni mkakati wa kumkomboa mkulima kutoka kwenye kilimo cha jembe la mkono na kumpeleka kwenye trekta bali na mipango mingine ni lazima ifanyike ili kumkomboa mkulima huyu. Ukame ndio huo umeshakuwa ni moja kati ya changamoto ambazo wakulima wanalia nazo lakini zipo njia mbadala ambazo zaweza kutumika ili mkulima aendelee na kilimo chenye manufaa. Mbali na hayo yote pia wapo wakulima waliojidhatiti katika kuzalisha mbegu zisizo na magonjwa kwa kutumia tussue kama afanyavyo Bwana Mushobozi wa Kisongo Arusha. Yeye huzalisha mbegu za migomba, mihogo, pamoja na mihogo ambapo Serikali ni lazima ichukuwe mkondo wake katika kuwasaidia watanzania waliojitolea kwa hali na mali katika kuwainua wakulima wadogo wadogo nchini.
mbegu za migomba zikiwa katika hatua ya awaali
mbegu za viazi vitamu pamoja na mihogo
Bwana Mushobozi akieleza kitu kwa waandishi kuhusiana na migomba
Maabara ya Bwana Mushobozi anayotumia kuzalisha tishu za mbegu
mbegu za migomba zikiwa bado zipo katika kifaa maalum kwa kuzalishia mbegu hizo
watanzania inabidi tuondokane na mtazamo duni wa kuongea na kupanga sana bila kuwa na utekelezaji vitu ambavyo ni ugonjwa mkubwa nchini. Msemo huu unakuja kutoka na kwamba wataalamu wengi wapo sana maofisini wakitoa maagizo bila ya kuwa mstali wa mbele katika utekelezaji. Viongozi wa serikali inabidi kuondokana na mtazamo wa kimazoea na kubadirika ili kufanya kazi zenye tija kwa jamii haswa katika sekta muhimu kama kilimo. Wapo mawaziri ambao hawajawahi hata siku moja kuwatembelea wakulima na kuwauliza matatizo yao kitu ambacho hakifai kabisa kutokea. Wapo wataalam na wakulima amboa wanatamani sana kama wangepewa nafasi ya kukutana na waziri wakilimo ili tu aseme nae neon lakini hawana nafasi hiyo. Viwanda kama TBL badala ya kudhamini burudani na mpira isisahau kuwa ngano na shairi ni mazao wanayoyatumia kuzalishia vinywaji, hivyo ni wajibu wao pia kudhamini tafiti za begu bora za mazao haya ili kuepukana na ghalama za kununua mazao hayo kutoka nje na badala yake wakulima wa ndani watalima na kuwanufaisha wao pia. hivyo basi ipo sababu ya kutazama na upande wa pili ili kuona nini chakufanya katika udamini. Wapo vijana ambao wanatamani kama wangelikuwa na pakuanzia na kufanya kitu kinachoonekana katika jamii lakini hawajui wapi wataanzia, lakini kumbe wakidhaminiwa wanaweza kuondokana na wimbi la mabaya ambalo linamaliza vijana amboa ndio nguvu kazi ya taifa letu
Mwandishi wa TBC Taifa Greyson Mutembei akimuhoji mtafiti wa gano na shairi Bwana Mamuya.
Shamba la ngano Serian
Shairi
Shamaba la ngano zilizo pandwa tofauti tofauti ili kupata mbegu bora
Hata hivyo waandishi wa habari hawakusita kutafuta undani wa habari kuhusu uwepo wa mbegu za GMO kitu kilichowafanya kwenda TPRI na kukutana na mkaguzi wa mimea chini ya wizara ya kilimo Bwana Oshingi Shilla ambaye aliwahakikishia kuwa mpaka sasa hakuna mbegu ya aina yoyote nchini ambayo ni ya vinasaba. Hata hivyo alisema kuwa GMO si kwa kila zao au kila mbegu bali kuna mazao ambayo ni sumbufu hayo ndiyo ambayo yatafanyiwa utafiti kuyaweka katika mfumo wa vinasaba na watafanya hivyo endapo watagundua kuwa mbegu hizo zittakuwa na manufaa kwa wakulima wenyewe pamoja na watumiaji kwa ujumla. Hata hivyo watoa elimu inabidi kufanya juhudi ili kuondoa mawazo mgando kwa watanzania wanaofikiri tofauti kuhusu jambo hili la vinasaba. Uhakika upo ya kuwa hakuna mbegu wala zao litakaloingia nchini bila utafiti wa kina na wanasayansi wazawa ili kuwa na uhakika zaidi na mazao hayo.
Bwana Oshingi Shilla (wa pili toka kushoto) akiongea na waandishi TPRI
Waandishi wa habari wkifuatilia kwa makini maelezo ya Bwana Oshingi Shilla
Mwisho wa siku kilimo kinabakia kuwa ndio uti wa mgongo wa Tanzania japokuwa juhudi zaidi zahitajika katika sekta hii. Kilimo pekee ndio sekta yenye ajira tosha kwa vijana wasiokuwa na ajira.
shamba la mauoa kwa ajili ya biashara nje na ndani ya nchi.
No comments:
Post a Comment