Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod
Slaa, amedai kuwa baadhi ya viongozi wa Serikali wamegawana na kutafuna
fedha zilitolewa na Benki ya Dunia, ili kugharimia miradi ya kuchimba
visima 10 vya maji katika kila wilaya nchini.
Dk Slaa alitoa tuhuma hizo juzi jioni,
alipokuwa akihutibia mkutano wa hadhara katika Uwanja wa Shule ya Msingi
Mkendo, mjini Musoma.
Kiongozi huyo wa Chadema yuko katika Operesheni ya M4C Pamoja Daima.
Alisema kitendo hicho kinafanywa wakati
Watanzania na hasa wanawake wakikabiliwa tatizo kubwa la kukosa huduma
za maji kiasi cha kushinda hata kwa siku tatu bila kuoga.
“Ngoja niwaambie hivi sasa Serikali
imekuwa ikiweka vikwazo vingi katika utekelezaji wa mradi wa maji
kupitia Benki ya Dunia, ukweli ni kwamba fedha zote zilizotolewa
zimeliwa sasa wameanza kuhaha wasijue cha kufanya,” alisema na kuongeza.
Wakati huohuo, Geofrey Nyang’oro na
Raymond Kaminyonge wanaripoti kutoka Iringa kuwa viongozi wa Chadema
Taifa wakiongozwa na mwenyekiti wake, Freeman Mbowe wamekamatwa na
polisi mkoani hapa na kushikiliwa kwa muda wakituhumiwa kuzidisha muda
katika mikutano waliyoifanya katika Jimbo la Kalenga wilayani hapa juzi.
Mbowe alikuwa ameambatana na viongozi wa
chama hicho juzi, walifanya mikutano mbalimbali mkoani hapa, ambapo
katika Jimbo la Kalenga walifanya mikutano katika Vijiji vya
Wassa,Nzihi, Kidamali na kisha kushindwa kufanya mkutano mmoja
uliotakiwa kufanyika katika Kijiji cha Mgama kwa madai muda ulikuwa
umekishwa.
Mwenyekiti huyo pamoja na viongozi
wawili wa Chadema, Mbunge Peter Msigwa na Halima Mdee walikamatwa saa
tatu asubuhi wakati mwenyekiti huyo alipokuwa akijiaandaa kuondoka
mkoani humo kwenda mkoani Pwani kuendelea na mikutano ya Operesheni M4C
pamoja Daima inayoendelea kwa sasa kote nchini. Hii ni mara ya pili kwa
kiongozi huyo kukamatwa na kuhojiwa ambapo mara ya kwanza ilikuwa
Agosti 25 mwaka jana.
No comments:
Post a Comment