MWENYEKITI
wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, amemvaa
Rais Jakaya Kikwete, akimtaka kuacha kutafuta huruma ya Watanzania juu
ya suala la Katiba na badala yake atumie nafasi hiyo kuwataka wabunge
wake kuheshimu maoni ya wananchi.
Mbowe ambaye
pia ni Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, alisema kuwa hotuba
ya Rais Kikwete juzi kwamba Katiba haiwezi kupatikana kwa ngumi imejaa
upotoshaji kwa wananchi.
Katika hotuba yake ya maadhimisho ya
miaka 37 ya kuzaliwa kwa CCM, yaliyofanyika mkoani Mbeya, Rais Kikwete
ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM, alimshangaa Mbowe kwa kauli yake kwamba
mfumo wa serikali tatu ukikataliwa katika Bunge hilo nchi
haitatawalika.
“Huku ni kuwadanganya wananchi, pale hakuna ngumi
wala vurugu yoyote, kila ibara iliyopo katika rasimu itajadiliwa ili
upatikane mwafaka. Huku ni kukosa ukomavu wa kisiasa,” alisema.
Akizungumza
na Tanzania Daima jana, Mbowe alisema ni vema Rais Kikwete akaacha
kuhangaika na wapinzani, badala yake awe tayari kuheshimu mawazo ya
wananchi waliyotoa wakati wa kutoa maoni ya Katiba.
Mbowe
alisema kuwa Rais Kikwete ni mwanasiasa na mtu anayejaribu kupotosha
hoja, kwani CHADEMA waliposema watapambana, hawakumaanisha kupigana
ngumi kama alivyosema kiongozi huyo.
Alisema kuwa viongozi wa
CCM wamekuwa wakilazimisha ajenda ya Katiba mpya kuonekana kama sera
yao, jambo ambalo CHADEMA haiwezi kuafiki.
“Katiba ni ya
wananchi, si ya chama chochote cha siasa, ndiyo maana hatukubali kuona
mawazo ya wananchi yakishindwa kuheshimiwa,” alisema.
Mwenyekiti
huyo alisema Tume ya Mabadiliko ya Katiba inayoongozwa na Jaji Joseph
Warioba imefanya kazi nzuri ambapo Rais Kikwete na wabunge wake
wanapaswa kuheshimu mchango huo.
Alisema kuwa CHADEMA
itahakikisha inashindana kwa hoja katika Bunge la Katiba litakaloketi
hivi karibuni na iwapo hilo litashindikana watarudi kwa wananchi ambao
ndio wenye uamuzi wa mwisho juu ya suala hilo.
“Wajumbe
watakaoshiriki Bunge la Katiba ni 640 ambao hao si waamuzi wa mwisho na
kama tutaona kuna suala lolote linaloenda kinyume, sisi tutakachokifanya
ni kurudi kwa wananchi kuwaeleza juu ya kilichotokea na hao ndio wenye
maamuzi ya mwisho katika kura ya maoni,” alisema.
Mbowe alisema
kuwa hata katika kushindana kwa hoja CCM wanapaswa wasiweke hila, maana
wataweza kuchangia mchakato huo kushindwa kufanikiwa.
Alisema
kuwa nia ya CHADEMA ni kuhakikisha Katiba nzuri, bora na iliyo ya
wananchi inapatikana na si kusababisha vurugu kama ambavyo Rais Kikwete
amejaribu kupotosha.
“Hila hiyo imeonekana wazi maana kuna hali
ya kutaka kupuuza mawazo ya wananchi na CCM kulazimisha mawazo yao, hilo
hatutalikubali na tutapambana…hiyo si mara ya kwanza kupambana katika
suala hilo,” alisema.
Mbowe alisema kuwa kuhusu serikali tatu ni
muhimu Rais Kikwete akaheshimu mawazo hayo na CHADEMA itashindana kwa
hoja juu ya suala hilo ili kuhakikisha mawazo hayo yaliyowasilishwa na
Jaji Warioba yanaheshimiwa.
Katika ziara ya mikutano ya hadhara
ya CHADEMA iliyopewa jina la Operesheni M4C Pamoja Daima, Mbowe na
viongozi wengine waliionya Serikali ya CCM kutochakachua mchakato wa
Katiba, kwani Watanzania hawako tayari kurudi kwenye Katiba ya sasa
ambayo alidai imekosa uhalali wa kuongoza nchi.
Alisema CCM kwa
kutumia wabunge wake wakiamua kuhujumu mchakato huo bungeni, yeye na
viongozi wenzake watapita nchi nzima kuwataka wananchi wasishiriki kura
za maoni na yuko tayari kufunguliwa kesi kwa kudai Katiba
No comments:
Post a Comment