Mbunge wa Singida Mashariki, mnadhimu wa
upinzani na mwanasheria mkuu wa CHADEMA mh. Tundu Lissu, amesema kuwa
wabunge wengi wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania hawajui lugha
ya kiingereza kitendo kinachowafanya wakose ufanisi katika kazi zao za
kibunge hususani mijadala mbalimbali bungeni na nje ya bunge.
Mwanasheria huyo amekiita kitendo hicho
kuwa ni janga la taifa ambapo ameshauri suala hilo litazamwe upya ili
tuwe na wabunge wanaoweza kuwa tija kwa taifa.
Ikumbukwe kuwa wabunge wengi wa bunge
hili wamekuwa wakituhumiwa kuwa na elimu za kidato cha nne (iv) au chini
ya hapo na wengine kidato cha sita chenye matokeo mabaya.
No comments:
Post a Comment