Bagamoyo. Mwinjilisti wa Kanisa la Anglikana
Kijiji cha Gama, wilayani Bagamoyo, Mkoa wa Pwani, anadaiwa kumuua mkewe
kwa wivu wa mapenzi, kwa kumpiga na panga kichwani kisha kumfukia chini
ya magogo aliyoandaa kwenye tanuri la mkaa porini.
Mwinjilisti huyo ambaye ni mkazi wa kijiji hicho,
licha ya kazi ya kueneza Injili pia ni mkulima na anajishughulisha na
shughuli za kuchoma mkaa porini.
Kamanda wa Polisi mkoani Pwani, Ulrich Matei
alithibitisha tukio hilo na kwamba mwanamke aliyeuawa ni Mboni Patrick
(28) mkazi wa kijiji hicho.
Matei alisema siku ya tukio Januari 20, saa 10:00
jioni Mwinjilisti huyo anadaiwa alitoka nyumbani akiwa na mkewe huyo na
mtoto wao, Sabina Gabriel (10) kuelekea porini kukata miti ya kuandaa
mkaa.
Matei alisema baada ya kukamilisha kukata miti,
wanandoa hao walimtuma mtoto kurejea nyumbani kupika chakula ili
wakimaliza kuwasha moto wakale.Alisema kuna dalili kuwa wakati mtoto
anaondoka ndipo mume alipochukua panga na kumkata mkewe upande wa kulia
kichwani, hivyo kuvuja damu nyingi.
“Baada ya kutekeleza mauaji hayo, baba huyo
alichukua mwili na kuuweka katika tanuri walilokuwa wameliandaa kwa
ajili ya mkaa na kuulaza chini, kisha kujaza magogo yote waliyokata na
kuanza kuwasha moto,” alisema Matei na kuongeza:
“Inaonekana lengo lilikuwa kumteketeza kabisa mkewe.”mama na zile kuni kwenye tanuri”alisema Matei.
Kamanda huyo alisema muda mfupi mtoto aliyetumwa
nyumani kupika alirudisha majibu porini ya chakula kuwa tayari lakini
hakuwakuta wazazi wake na alianza kuita huku na kule bila mafanikio na
ghafla ndipo alipoona damu nyingi imetapakaa jirani na tanuri na
kufatilia akaona mkono ukichungulia kwenye tanuri la mkaa, huku damu
ikichuruzika eneo hilo.
Alisema hali hiyo ilimpelekea mtoto kupiga yowe na
kukimbilia kijijini na ndipo wanakijiji wakajitokeza na kuanza kuelekea
eneo la porini na kukuta mwili wa mama huo ukiwa umefukiwa chini ya
magogo ya mkaa kwenye tanuri huku ikivuja damu nyingi wakautoa na kuanza
msako wa baba ambapo walimkuta ameshakufa kwa kujinyonga na mwili wake
ulikua bado ukining’inia juu ya mti umbali wa mita 500 .
“Uchunguzi wetu wa awali ni kuwa Muinjilisti huyo
hivi karibuni alipata taarifa kuwa mke wake ana mahusianao na mtu
mwingine hali ambayo ilimuingizia msongo wa mawazo na bila ya kufatilia
ndipo alipokubwa na shetani huyo na kuchukua hatua hiyo, kwa hiyo
kiujumla sababu ya hili tukio ni wivu wa “alisema Matei.
No comments:
Post a Comment