Pages

Translate

Tuesday, 21 January 2014

MAMA LULU, MAMA KANUMBA WAENDA KULA KIAPO


Lucresia Karugila ‘Mama Lulu
  
ULE udugu wa ukubwani kati ya wazazi wa mastaa wa filamu Bongo, Lucresia Karugila ‘Mama Lulu’ na  Flora Mtegoa ‘Mama Kanumba’ umezidi kukua kufuatia kwenda Bukoba, Kagera kwa ajili ya kula kiapo cha kuimarisha undugu huo.


Kutoka kushoto: Flora Mtegoa, Lulu na Lucresia Karugila katika pozi.
 
Wazazi hao wawili walijikuta katika undugu kufuatia Elizabeth Michael ‘Lulu’ kupata mkasa wa kifo cha aliyekuwa nyota wa filamu, marehemu Steven Kanumba kilichotokea Aprili 7, 2012.
Lulu alidakwa akihusishwa na kifo hicho na kuswekwa mahabusu mpaka mwaka jana alipoachiwa kwa dhamana na mahakama kuu huku kesi hiyo ikiwa kwenye mchakato wa kuanza kusikilizwa.
Tangu kuachiwa kwa Lulu, Mama Kanumba amekuwa karibu na staa huyo akisahau yaliyotokea. Ukaribu wa Mama Kanumba kwa Lulu ukajikuta ukiunga moja kwa moja kwa mama wa Lulu ambapo wote watangaza wamekuwa ndugu.


Akizungumza na gazeti hili juzi jijini Dar, Mama Lulu alisema yeye na Mama Kanumba wanaondoka leo (Jumanne) kwa ndege kwenda Bukoba ambako, mbali na kumuuguza  mama mzazi wa Mama Kanumba ‘Bibi Kanumba’, lakini pia wataitumia nafasi hiyo kula kiapo cha kimila ili udugu wao uwe wa damu.

“Tunaondoka Jumanne kwa ndege, tunakwenda Bukoba. Kule kuna kumjulia hali bibi wa Kanumba ambaye anaumwa, lakini pia tutaitumia nafasi hiyo kula kiapo cha kimila ili undugu wangu na Mama Kanumba udumu mpaka kifo,” alisema Mama Lulu.
Kuhusu kuwepo madai kwamba, yeye na Mama Kanumba wapo ndani ya bifu zito, Mama Lulu alikanusha akisema haitatokea.

Flora Mtegoa ‘Mama Kanumba’.
 
“Mimi na Mama Kanumba tuwe na bifu? Haitatokea. Ndiyo maana tumefikia hatua hiyo ya kula kiapo cha kimila,” alisema Mama Lulu.
Kwa mila na desturi za makabila mengi Tanzania, watu wanapopenda kiasi cha kula kiapo kuwa ndugu (yamini) kila mmoja huchanjwa kidole kisha kuunganisha na cha mwenzake huku damu zikitoka.
Baada ya hapo, kila mmoja hunyonya kidole hicho chenye damu tendo ambali huaminika kuwa ndilo huunganisha undugu kuwa kama wa damu. Wazazi hao wote ni wenyeji wa Mkoa wa Kagera.

No comments:

Post a Comment