Usione vyaelea: Sharobaro (katikati) akilia baada ya kuchezea kichapo kwa kukutwa na mke wa mtu.
Tukio
hilo lilijiri saa saba usiku mwishoni mwa wiki iliyopita, Chalinze
mkoani Pwani ambapo mapaparazi wetu walikwenda kwa ajili ya uzinduzi wa
kundi jipya la sanaa liitwalo 3 Ways.Wakati shamrashamra zikiendelea, ghafla liliibuka timbwili na katika kufuatilia ilibainika sharobaro anayeishi eneo hilo alikuwa akila kipigo kutoka kwa mwanaume mmoja akimtuhumu kuwa alimkuta akiwa amekaa chobingo kihasarahasara na mkewe.
Mke wa mtu sumu: Sharobaro hoi baada ya kipigo.
Licha
ya baadhi ya wasanii kujaribu kuingilia kati ugomvi huo, jamaa
huyo aliendelea kushusha kichapo hadi pale watu walipomtolea uvivu na
kumzuia asije akasababisha mauaji.“Unajifanya sharobaro halafu unazengea wake za watu, sasa wee umeipata fresh na huyo mwenzako akirudi nyumbani naye
atakiona,” alisikika akisema mwanaume huyo huku akionekana kufura.
Kufuatia kichapo hicho, sharobaro huyo alijikuta akiangua kilio huku akilalama kuwa mwanamke huyo amemponza na kumharibia siku yake.
Kilio: Sharobaro akizidi kububujikwa na machozi baada ya kipondo kutoka kwa mwenye mali.
Wakizungumzia
tukio hilo, baadhi ya mashuhuda walisema, kipigo alichopata kijana huyo
ni fundisho kwa masharobaro wengine ambao wamekuwa na uhusiano
wa karibu na wake za watu.“Unajua hawa vijana hii ndiyo dawa yao, wanajisahau sana. Yaani anajua kabisa fulani ni mke wa mtu lakini anajiweka, sasa kwa kipigo hiki atakuwa fundisho,” alisema baba mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Baba Zulfa.
Aidha, wengine walimtetea kijana huyo na kudai kuwa mwanamke huyo ndiye anayestahili kulaumiwa kwa kukubali kukaa gizani na kijana huyo
No comments:
Post a Comment