Pages

Translate

Wednesday, 2 October 2013

HII NAYO NI TEKNOLOJIA YA JUU KABISA

MCHINA AOTESHWA PUA KWENYE PAJI LA USO ILI IKIKUA IWEKWE BAADA YA PUA HALISI KUHARIBIKA...



Mchina aoteshwa pua nyingine kwenye paji lake la uso. Mchina huyo ambaye anatumia jina moja tu la Xiaolian, alipata matibabu ya kuunda pua ambayo itakaa badala ya pua yake halisi ambayo iliathirika na kuharibika.
Taratibu zilifanyika katika hospitali iliyoko Fuzhou huko Fujian
Mwanaume huyo mwenye miaka 22 aliharibu pua yake kwenye ajali ya gari Agosti 2012 lakini alishindwa kupata matibabu
Matokeo yake  pua yake ikaathirika mpaka wale madaktari wakashindwa kuirekebisha.
Hawakuwa na jinsi nyingine yeyote ila kumuotesha pua nyingine alafu kuiondoa baadae ili iwekwe pale ambapo pua halisi iliharibiwa.

Pua hiyo ilitengenezwa kwa kuweka tissue expander za ngozi kwenye paji la uso la Xiaolian.Ilikatwa kwenye shepu ya pua na ikawa imehimarishwa na cartilage iliyotolewa kwenye mbavu zake.
Madaktari hao wa oparesheni wamesema kuwa pua hiyo imekua vizuri na oparesheni ya transplant itafanyika hivi karibuni

Ila mh! Kweli hii nose job! Mchina ana pua nyingine kwenye paji la uso kuireplace pua halisi iliyoharibika kwenye ajali ya gari....!!

No comments:

Post a Comment