JESHI la Polisi mkoani Dodoma limeshindwa kumpandisha kizimbani Mbunge
wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi (CHADEMA), kwa madai kuwa upelelezi bado
haujakamilika.
Mbilinyi, maarufu kama ‘Sugu’ alifunguliwa jalada na jeshi hilo Ijumaa
iliyopita, akidaiwa kumjeruhi jichoni askari wa Bunge, Koplo Nikwisa
Nkisu.
Akizungumza na waandishi wa habari jana mjini hapa, Wakili wake, Tundu
Lissu, alisema kuwa hawakufikishwa mahakamani kama walivyotegemea
kutokana na kuelezwa kuwa upelelzi haujakamilika.
Lissu ambaye ni Mbunge wa Singida Mashariki, alisema kuwa baada ya mteja
wake kuripoti kituoni aliambiwa kwamba upelelezi huo ukikamilika
wataitwa ili kupewa maelezo ya hatua gani inafuata.
Alisema kitendo hicho cha polisi kuwaita bila kukamilisha upelelezi wao ni kuwapotezea muda.
“Nashangaa ni kwanini tunaitwa, tuliambiwa tufike hapa, lakini
tulipokuja hapa hakuna jambo lolote la maana tuliloambiwa, badala yake
wanasema tuendelee na shughuli zetu upelelezi haujakamilika na baada ya
wiki mbili watatuambia kinachoendelea.
“Yaani, haya mambo yanayofanywa na serikali ya Chama Cha Mapinduzi na
Naibu wa Spika, Job Ndugai, ni ya ajabu sana. Tumeitwa kutoka mbali kote
kwa ajili ya kuja hapa kuambiwa kuwa upelelzi haujakamilika,” alisema.
Aliongeza kuwa Sugu alitoka Mbeya huku naye akitoka huko alikokuwa kwa
ajili ya kuja Dodoma lakini hakuna jambo lolote limefanyika, na kuhoji
ni kwanini wasingearifiwa hata kwa simu.
Lissu alisema kuwa atashanga kama jeshi hilo litapeleka kesi hiyo mahakamani kwani kosa lenyewe lilifanyikia bungeni.
“Nitashangaa kama jambo hili litapelekwa mahakamani, kwani kwa mujibu wa
kanuni, mbunge hatashitakiwa kwa jambo ambalo alilitenda akiwa katika
maeneo ya Bunge.
“Mambo haya yalitokea tukiwa bungeni na huko kuna kinga ya mbunge.
Mbunge akikosa anahukumiwa kwa mujibu wa kanuni, lakini kwa fikra na
mashikinizo ya viongozi wa CCM wanataka kuvuruga na kufanya mambo kwa
masilahi ya chama chao,” alisema.
Naye Sugu alisema kuwa kitendo kilichofanywa na Ndugai ni cha kihuni na
wala hakikuwa na misingi yoyote hadi kulazimisha askari wa Bunge kumpiga
Aidha katika hatua nyingine mitandao mbalimbali ya kijamii nchini Kenya
imeonesha kusikitishwa na udhalilishaji aliofanyiwa Mh; Sugu.
Wananchi Mkoani Mbeya na mikoa mingine wamesema wanatamani uchaguzi mkuu
ufike haraka ili watoe hukumu kali kwa Chama Tawala kwani wanashauhudia
kila kinachofanyika mjengoni huko na wanaamini vyombo hivyo vya dola
vinatumiwa kisiasa kwa manufaa ya mabosi zao waliowapa ajira.
No comments:
Post a Comment