 MTOTO Kudra akinyonya ziwa la mamaye.
MTOTO Kudra akinyonya ziwa la mamaye.
DAR ES SALAAM.
MTOTO Kudra aliyekuwa ameunganika na kiwiliwili cha pacha mwenza, anaendelea vizuri na matibabu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).
                
              MTOTO Kudra aliyekuwa ameunganika na kiwiliwili cha pacha mwenza, anaendelea vizuri na matibabu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).
Mtoto huyo alifanyiwa upasuaji Alhamisi iliyopita 
katika Taasisi ya Mifupa ya Muhimbili (Moi) na kulazwa katika wodi ya 
wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu (ICU), lakini mwishoni mwa wiki 
iliyopita alitolewa katika wodi hiyo.
                
              
Mama mzazi wa mtoto huyo, Pili Hija, alisema hivi 
sasa Kudra ananyonya vizuri na kwamba amekuwa akitaka kufanya hivyo kila
 wakati.
                
              
“Kwa kweli kudra za Mwenyezi Mungu ndizo zimemweka
 hai mpaka leo hii, nilikuwa nimeshakata tam
aa kuwa nampoteza mwanangu, nazidi kumuomba Mungu amwekee mkono wake apone kabisa,” alisema Hija.
                
              aa kuwa nampoteza mwanangu, nazidi kumuomba Mungu amwekee mkono wake apone kabisa,” alisema Hija.
Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Watoto katika 
Hospitali ya Muhimbili, Dk Zaitun Bokhary, alisema mtoto huyo anaendelea
 vizuri na mwishoni mwa mwezi huu atafanyiwa upasuaji mwingine.
                
              
“Tunamwacha achangamke kwanza, mwishoni mwa mwezi 
huu tutamfanyia upasuaji mwingine wa kumwekea njia ya muda ya kutolewa 
haja kubwa, kwa kumpasua ubavuni baada ya hapo ataruhusiwa kwenda 
nyumbani,” alisema Dk Bokhary.
                
              
Kudra alipewa jina hilo Alhamisi usiku, saa kadhaa
 baada ya upasuaji kufanyika chini ya jopo la madaktari saba, 
walioongozwa na Dk Hamis Shaaban, mtaalamu wa Ubongo na Uti wa Mgongo 
kutoka Moi.
                
              
Alizaliwa Agosti 18, baada ya mwanamke huyo 
kujifungulia nyumbani watoto pacha, huku mmoja akiwa hajakamilika viungo
 vyote. Pia, kiwiliwili kilichoungana hakikuwa na kichwa, macho, maini, 
figo ila alikuwa na mshipa mmoja wa fahamu ambao ulikuwa umeshikana na 
mwenzake na kulazimisha madaktari hao kumfanyia upasuaji. MWANANCHI
 
 
No comments:
Post a Comment