Jitihada za kurejesha heshima kwa viwanja vya ndege nchini zilizoanzishwa na waziri wa uchukuzu Dk. Harisson Mwakyembe zinaonekana kuzaa matunda baada ya mwanadada kutoka nchini Nigeria Anthonia Ojo (25) kukamatwa na kete 99 za madawa ya kulevya dar es salaam leo.
Mwanamke  huyo amekamatwa  akieleke Roma Italia kupitia Paris Ufaransa 
kwa ndege ya Ethiopian Airways  na  aliingia hapa nchini 
Agosti 30 akitokea Nigeria. 
Kwa mujibu wa Kaimu Kamanda wa Viwanja vya 
Ndege, Renatus Chalya, Ojo ataendelea kubaki chini ya ulinzi wa polisi 
kwa uchunguzi zaidi, wakati madawa hayo yamepelekwa kwenye  ofisi ya mkemia 
Mkuu wa Serikali ili kubaini aina ya dawa hizo  na   thamani yake... 
 












 
No comments:
Post a Comment