Pages

Translate

Thursday, 19 September 2013

MGANGA ASABABISHA MGUU WA DEREVA BODA BODA KUOZA








  






Haya ni mateso anayopata Dereva mmoja wa boda boda mkazi wa Kimara King’ongo jijini Dar es Salamaa anayejulikana kwa jina la Joseph Nyunza, yupo katika mateso makali yaliyosababishwa na Sangoma aliyeng’oa vyuma alivyowekewa hospitalini na kusababisha mguu wake kuoza
 Akizungumza kwa uchungu akiwa hoi kitandani nyumbani kwa shangazi yake, Joseph alisema awali alikuwa dereva wa pikipiki lakini Julai mwaka huu, alipata ajali maeneo ya Kimara Suka jijini Dar es Salaam baada ya kugongwa na gari lililohama njia na kumvunja mguu wake wa kulia.


Baada ya kupata ajali hiyo, alikimbizwa Hospitali ya Taifa Muhimbili ambako alipokelewa na kupelekwa katika kitengo cha mifupa (Moi) ambako baada ya kufanyiwa vipimo, iligundulika kuwa mfupa mkubwa wa mguu wake ulivunjika, hivyo kuwekewa vyuma ‘antena’ ili uweze kuunga. Aliruhusiwa kurudi nyumbani huku akitakiwa kurejea tena hospitalini kwa ajili ya upasuaji.

Baada ya kurejea nyumbani na kukaa wiki kadhaa huku akitembelea magongo, alikosa fedha za kurudi hospitalini kwa ajili ya upasuaji ndipo alipojitokeza mganga wa jadi aliyemtaja kwa jina la Mama Sura aliyeahidi kumponya kidonda hicho.

Mganga huyo alimpaka dawa zake kwa siku kadhaa lakini hakuona nafuu yoyote. Kuona hivyo, Sangoma huyo alishauri kuondolewa kwa vyuma hivyo vya kitaalamu vingeuwezesha mguu huo kuunga vizuri.

“Kweli, siku iliyofuata mganga wangu alikuja na mtu mwingine, akanitoa vyuma bila ganzi, niliumia sana lakini nilivumilia kwa sababu alinihakikishia ningepona.

“Kadiri siku zinavyozidi kwenda ndiyo mguu unazidi kutoa wadudu wa chooni, jamani ninaomba mnisaidie Watanzania wenzangu, ninateseka sana mimi,” alisema Joseph.

Alisema baada ya kutolewa vyuma hivyo, aliendelea kupakwa dawa hizo za kienyeji kiasi kwamba hadi sasa mguu umeoza na unatoa funza huku kijana huyo akiwa hawezi hata kunyanyuka kitandani.


MGANGA ANASEMAJE?
Baada ya mapaparazi wetu kuzungumza na Joseph walimtafuta mganga huyo ambaye pia anaishi maeneo ya King’ong’o, hakuwepo nyumbani lakini alipatikana kwa njia ya simu.

“Mimi sijamkuta na hali hiyo aliyonayo sasa, naamini anaendelea vizuri na atapona kwa sababu nimeshawatibu watu wengi sana wa aina hiyo, mbona sasa hivi ana nafuu, muulizeni mwenyewe atawaambia,” alisema

MWENYEKITI ANENA
Naye Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa King’ong’o, Demetrius Mapesi amekiri kupokea taarifa hizo kwa masikitiko na kuanzisha harambee ya kumsaidia kupitia namba 0654 880707.

No comments:

Post a Comment