Pages

Translate

Thursday, 19 September 2013

FUNDISHO

NDOA YASAMBARATIKA KANISANI DAKIKA CHACHE KABLA YA KUIDHINISHWA

Hili  ni  tukio  la  kusikitisha, lakini  lenye  mafunzo  Mengi  ndani  yake.Tukio  hilo  lilitoke  mwanzoni  mwa  mwezi wa  nane  mwaka  huu ndani  ya  kanisa  la Pentekoste  la  nchini  Kenya  ambapo  wanandoa  wawili    walikuwa  wakila  kiapo  cha  maisha  mbele  ya  mchungaji  wa  kanisa hilo.


Dakika  chache  kabla  ya  wanandoa  hao  kuapishwa  na  kuruhusiwa  kuvishana  pete, Mchungaji  wa  kanisa  hilo   aliwauliza  waumini  kama  kuna  yeyote  mwenye  pingamizi  la  kufungwa  kwa  ndoa  ya  wapenzi  hao...

Baada  ya  swali  hilo, mwanamke  mmoja  alisimama  na  kuelekea  mbele  ya  kanisa  hilo  huku  akiwa  na  vyeti  mkononi.

Alipomkaribia  mchungaji, mwanamke  huyo  alipaaza sauti  yake  na  kusema  kuwa  ndoa  hiyo  haistahili  kufungwa  kwa  sababu  yeye  na  bwana  harusi  wanamtoto  waliyemzaa  pamoja  na  kwamba  walikuwa  na  mipango  ya  kuoana....

No comments:

Post a Comment