Mbakaji ambaye alifungwa jana anasubiria vipimo kubaini kama ameathirika na virusi vya ukimwi kutoka kwa muathirika aliye mbaka.
Richard Thomas, mwenye umri wa miaka 27,
 alianguka chini pale polisi walipomtaarifu kuhusu hali ya afya ya 
mwanamke huyo na anasubiria kusikia kama ameathirika na virusi hivyo 
visivyotibika.
Thomas, mkazi wa Leigh huko Greater 
Manchester, alimfahamu mwanamke huyo na alijua kwamba ana ugonjwa 
mwingine lakini hakuwa akijua kuhusu virusi vya ukimwi. Mahakama 
ilielezwa alishitushwa pale alipotakiwa kupelekwa hospitali, Mahakama 
Kuu ya Liverpool ilielezwa.
Alijipeleka nyumbani kwake katikati ya usiku na  mwanamke huyo akazinduka usingizini na kukuta Thomas akimbaka.
"Alitulia na hakuna aliyemwongelesha mwenzake. Alipangisha kaptula yake na kuondoka," alisema mwendesha mashitaka Harry Pepper.
"Alikamatwa na kuhojiwa na alisema 
alikuwa amelewa kupita kiasi, kutumia cocaine na kurukwa akili na 
hakuweza kukumbuka tukio hilo," aliongeza.
Wakili wake, Virginia Hayton, alisema 
kwamba bado hawezi kukumbuka shambulio hilo lakini alipoelezwa kuhusiana
 na hilo alisema kwamba mwanamke huyo 'hawezi kusema uongo, anaeleza 
ukweli. Kama anasema nimefanya hivyo, basi nimefanya'.
Akimfunga Thomas miaka mitano na miezi 
minne jela Jaji Mark Brown alisema kwamba amefanya 'kosa hili 
lisilopendeza' wakati mwanamke huyo akiwa amelala fofofo, akiwa amemeza 
vidonge vya usingizi, na ilimwacha akiwa mwenye mateso na wasiwasi.
Pia alimwamuru Thomas kusaini Rejista ya
 Wahalifu wa Kujamiiana kwa maisha. Thomas alipatikana na hatia ya 
kumbaka mwanamke huyo Julai 20 mwaka huu.
Hayton alisema kwamba Thomas, ambaye 
hapo kabla alishawahi kutiwa hatiani lakini si kwa makosa ya ubakaji, 
'katili' na 'hawezi kuelewa kwanini alifanya vile na inamsumbua mno'.
Alisema kwamba alianza kutumia bangi 
akiwa na umri wa miaka tisa, kunywa pombe kupita kiasi akiwa na umri wa 
miaka 11, kutopea dawa za kulevya hadi kufikia kurukwa akili na cocaine 
akiwa na umri wa miaka 13 na aliwekwa chini ya uangalizi maalumu mwaka 
uliofuata.
Amekuwa akijaribu kuwasiliana na familia
 yake lakini hawataki kufanya chochote kumsaidia na sasa atakuwa mbali 
na mpenzi wake na binti yao mdogo na mabinti zake wengine wawili wakubwa
 aliowapa katika mahusiano yake ya awali.
Hayton aliieleza mahakama hiyo kwamba 
Thomas hawezi kupata majibu ya vipimo vyake vya virusi vya ukimwi hadi 
Ijumaa na amekuwa na hofu kubwa ya matokeo hayo.
"Ni kosa lake mwenyewe, kama asingefanya kosa hili asingejiweka mwenyewe mahali hapa."
 

 
No comments:
Post a Comment