Mr Whittall, ambaye ni mkurugenzi wa
hoteli hiyo alisema kuwa mamba huyo aliingia kwa siri chumbani kwake na
kukaa chini ya kitanda chake usiku na kugundulika asubuhi ya siku
iliyofuata.
Alisema kuwa mamba huyo alitoka nyuma
ya pori lililopo karibu na hoteli hiyo ambapo hata yeye alipoamka
hakumuona na alining’iniza miguu yake huku mamba huyo akiwa chini ya
kitanda ambapo alitoka kwenda kupata kifungua kinywa kwenye mgahawa wa
hoteli hiyo.
Inaelezwa kuwa mamba huyo aligundulika
na mfanyakazi aliyekuwa akifanya usafi katika chumba hicho na kupiga
mayowe yaliyomshtua Mr Whittall ambapo alitoka mbia kwenda kushuhudia
kulikoni na kumkuta mamba huyo akiwa chini ya kitanda chake kumbe
alilala naye kwenye chumba hicho usiku mzima.
Mamba ni wataalam wa kujificha na
ndiyo maana hunusirika kuuwawa na wanyama wengine hususani binadamu
hata wakiwa nje ya maji,alisema Mr Whittall.
Na huweza kutulia sehemu moja kwa muda
mrefu bila kugundulika na myama yoyote hivyo kumtambua inakuwa ni
vigumu hiyo ni kutokana na maumbile yao yalivyo na hukimbilia ndani ya
vichaka au kuingia kwenye nyumba kama hotelini hapo kufuata joto hasa
katika kipindi cha mvua na baridi kali na alipenda kukaa chini ya
kitanda hicho kwasababu kulikuwa na joto.
Mkurugenzi huyo alilazimika kuwaita
wafanyakazi wengine ambao walisaidiana kumuondoa mamba huyo kutoka
kwenye chini ya kitanda na kumtupa kwenye bwawa la hoteli hiyo.
No comments:
Post a Comment