Mrembo Yusta Mkali, mkazi wa Kawe, Dar
ambaye alikuwa mke wa mtu anadaiwa kuuawa kwa kutobolewa koromeo na
mumewe, Musa Senkando na kusababisha simulizi ya kutoa machozi kisa
kikielezwa kuwa ni wivu wa kimapenzi.
Polisi wa kituo cha Kawe wakiukagua mwili wa marehemu Yusta.
Mauaji hayo ya kikatili yalitokea wiki
iliyopita maeneo ya Kanisani Kawe, Dar usiku wa kuamkia Ijumaa ambapo
mwili wa marehemu ulikutwa ukiwa na jeraha kwenye koo huku mwanaume huyo
akiwa hajulikani aliko baada ya kufanya mauaji hayo.
Habari kutoka eneo la tukio zilieleza
kuwa Musa alikuwa akimfanyia visa mkewe huyo mara kwa mara ambapo mwaka
jana alimpiga na kumchana mkono.
Mtuhumiwa wa mauaji, Musa Senkando.
Ilidaiwa kuwa aliwahi kumpiga na stuli lakini alijikinga kwa mkono ili asiumie sehemu za kichwani.
Uchunguzi wa awali ulionesha kuwa muuaji alitumia kitu chenye ncha kali ambacho alimshambulia nacho kwenye koromeo.
Marehemu ameacha mtoto mmoja anayejulikana kwa jina la Joshua Zebedayo.
Mwili wa marehemu Yusta ukipelekwa kuhifadhiwa katika Hospitali ya Mwananyamala.
Ilielezwa kuwa Joshua ndiye aligundua
kuwa mama yake amekufa baada ya kuingia chumbani kwa lengo la kufanya
usafi lakini alishangaa kumuona mama yake akiwa amelala huku amefunikwa
shuka na alipojaribu kumuita hakuitika ndipo akamfunua na kukutana na
mwili ukiwa umejaa damu.
Marehemu Yusta Mkali enzi za uhai wake.
Mtoto huyo alipiga kelele akiomba msaada ambapo watu walijaa na kushuhudia mwili wa mwanamke huyo na kusababisha vilio kutawala.
Wakazi wa Kawe wakiwa na simanzi wakati mwili wa marehemu ukipelekwa hospitali.
“Huu ni unyama wa ajabu sana. Haya
mapenzi ni ya kuyatazama sana. Ona sasa mwanaume amemuua mkewe. Inauma
sana,” alisema mama Jack ambaye ni jirani wa familia hiyo.
Mtoto wa marehemu aitwaye Baraka Simon akiaga mwili wa mama yake kwa simanzi jana.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Dar, Camilius Wambura alithibitisha kutokea kwa tukio hilo.
Mwili wa mwanamke huyo ulihifadhiwa katika Hospitali ya Mwananyama na mtuhumiwa anasakwa kujibu tuhuma zinazomkabili.
Ilikuwa ni simanzi na majonzi wakati wa
kuaga mwili wa marehemu Yusta, jana katika Hospitali ya Mwananyamala
jijini Dar kabla ya kuusafirisha kwenda mkoani Dodoma kwa mazishi.
No comments:
Post a Comment