Pages

Translate

Sunday 11 August 2013

MAPENZI NAYO YASABABISHA MAAFA KILA UCHWAO: DEREVA BODABODA AUAWA KIKATILI AKATWAKATWA MAPANGA KISA WIVU WA MAPENZI

 
  MWENDESHA bodaboda mkazi wa kijiji cha Igalako wilayani Mbarali, Mbeya, Yohana Mkinga (17) ameuawa kwa kupigwa mapanga na kisha mwili wake kutelekezwa kwenye shamba la mpunga katika tukio linalohusishwa na wivu wa kimapenzi.

Tukio hilo limethibitishwa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya, Diwani Athumani amesema kuwa, mwili wa marehemu ulikuwa na majeraha ya kukatwa mapanga, huku vidole viwili vya mkono wa kushoto vikiwa vimenyofolewa. Kamanda huyo ameongeza kuwa, jicho lake la kushoto la kijana huyo lilitobolewa na kutolewa. Aidha, mwili umekutwa na majeraha manne makubwa kichwani.

Alisema Mkinga ambaye aliondoka nyumbani kwake jioni ya Jumatano wiki hii akiwa na pikipiki aina ya Shinley yenye namba za usajili T770 BYH, mwili wake ulionekana siku mbili baadaye katika kijiji cha Muhela, Mbarali ambako pia pikipiki ilitelekezwa.

Aliongeza kuwa, uchunguzi wa awali unaonesha kuwa, kijana huyo ameuawa kutokana na wivu wa mapenzi,u juhudu za kuwasaka wahusika wa mauaji hayo zikiendelea.

Katika tukio jingine, Tegemeo Wilangali (29) ambaye ni mkulima wa kijiji cha Mwakaganda wilayani Mbarali, amekufa baada ya kukanyagwa na trekta alilokuwa analidandia likiwa katika mwendo kasi.

Kamanda Athumani amesema ajali hiyo ilitokea juzi kijijini hapo. Trekta hilo lenye namba za usajili T 885 BPY, likiwa na tela ambalo halina namba za usajili, lilikuwa likiendeshwa na Alex Kalonga (25), mkazi wa Ubaruku

No comments:

Post a Comment