Pages

Translate

Friday, 23 August 2013

KAULI YA MWASITI KUHUSU ALICHOKISEMA NEY WA MITEGO KWAMBA KIGOMA ALL STARS IMEKUFA



Leo hii msanii na muhasibu wa Kigoma All Stars,  Mwasit Almasi a.ka Mwasiti amezungumza juu ya tuhuma za rapper Ney wa mitego kupitia wimbo wake "nasema nao" kuwa Kigoma All Stars imekufa.
  

  mwasitiamesema"Hahahaaa jamani, unajua mi siendi kujibu hizi mambo, mi sipendi hizo maneno maneno
kurushiana,lakini mi nataka watanzania wajue kitu kimoja, safari hii simjibu Ney, najibu watanzania kwasababu wao ndio wamepelekewa ujumbe, nawaambia watanzania kwamba Kigoma All Stars ni kampuni sio group ya mziki, kigoma all stars ni kampuni ya wanamziki, ingekuwa ni group wangekuwa wanatuona tunafanya kazi wote kila sehem sasa hivi, ile ni kampuni ya wanamziki ambao wanashughuli zao, huwezi kukuta hiyo group nzima iko kwenye  mkoa mmoja inafanya show mfano Fiesta, ni ngumu, ile mtu akipelekwa ni kazi yake binafsi , lakini tukimuhitaji kwenye kazi ya kampuni tutampata, kwahiyo hakuna kitu kinachoitwa kufa kwa kigoma all Stars, kigoma all stars ni kampuni ambayo kila mwana mziki ana share katika ile kampuni, kwahiyo ni ngumu kufa, kila mwanamziki amewekeza pale, kila mwanamziki anajua hapa nina changu kwahiyo ni yake"

No comments:

Post a Comment