Mbakaji
Erasto Mwakyomo (50) anayetuhumiwa kwa ubakaji akiwa akiwa katika ofisi ya mwenyekiti wa mtaa wa mapelele kabla ya kuchukuliwa na mwenyekiti wa dawati la watoto na ukatili wa kijinsia Bi. Mary Gumbo
Mwenyekiti wa mtaa CHRISTOPHER MWAKIBETE
Baadhi ya ndugu na wazazi ya watoto wakiwa nyumbani kwa mwenyekiti wa mtaa
ERASTO
MWAKYOMA mwenye umri wa miaka hamsini mkazi wa mtaa wa Mapelele Kata ya
ILEMI jijini Mbeya anahojiwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za
kuwadhalilisha watoto wawili wa kike wote wakazi wa Mapelele.
Wazazi
wa watoto hao baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa watoto hao ambao
mmoja ana umri wa miaka minne na mwingine mitano walitoa taarifa kwa
Balozi wa mtaa Bwana CASIAN MWEZIMPYA ambapo baada ya kutafakari kwa
kina aliamua kulipeleka suala hilo kwa Mwenyekiti wa Mtaa.
Mwenyekiti
wa mtaa Bwana CHRISTOPHER MWAKIBETE Aliamua kuwaita wazazi na mtuhumiwa
kuwahoji yaliyotukia ambapo nao watoto walipewa nafasi ya kueleza ambao
walieza kuwa ERASTO Alikuwa akiwashika sehemu za siri na kuwapaka
mafuta kabla ya kufanya nao mapenzi.
Baada
ya kusikiliza kwa makini MWAKIBETE aliamuru kuwa suala hilo ni la
kisheria na kitaalamu hivyo hawezi kuchukua hatua zozote bali suala hilo
analazimika kulipeleka Polisi ambapo Mwenyekiti wa Dawati la watoto na
jinsia MARY GUMBO Alimchukua mtuhumiwa hadi kituo cha Polisi kati.
Baada
ya mahojiano ya awali GUMBO aliwachuchukua watoto hadi Hospitali ya
Rufaa kwa uchunguzi na mtuhumiwa kubaki kituo cha kati kwa mahojiano
zaidi,hata hivyo uchunguzi umebaini kuwa baadhi ya watoto mtaani hapo
wamekuwa wakitendewa vitendo vya ukatili lakini vimekuwa vikifumbiwa
macho na baadhi ya wazazi wakihisi ni aibu kwa watoto wao.
No comments:
Post a Comment