Kwani ni njia pekee ya mafanikio katika kilimo
Hayo yamesemwa na bi Rose Mongi ambaye ni mtafiti na mtaalamu wa ngano na maharage katika kituo cha utafiti na kilimo Uyole mkoani Mbeya ARI. Amesema wakulima wengi hawajapata mazao kama walivyokuwa wakitarajia kutokana na wao wenyewe kutokuzingatia kanuni na njia bora za kilimo ambazo wanatakiwa kuzifuata ili kupata mafanikio makubwa katika kilimo. Japo kuwa kulikuwa na mvua za kutosha sehemu nyingi za nyanda za juu kusini laikini wakulima wengi wamepata mavuno machache kutokana na mfumo wanaoutumia wakulima wenyewe. Pia amesema kuwa wakulima wengi siku hizi wamekuwa wakaidi wa kufuata kanuni hizo kutokana na kuwa na propaganda nyingi katika sekta ya kilimo, akidai kuwa hiyo ni changamoto kati ya changamoto nyingi nambazo zinaikabili sekta ya kilimo Tanzania.
Bwana Anthon Elanga msaidizi wa Bi Rose katika utafiti
Rose Mongi mtafiti wa mbegu za ngano na maharage ARI Uyole Mbeya
Bi Rose amesema kuwa wao kama wataalamu wapo kwa ajili ya wakulima ili wawatumie vile watakavyo, "sisi kama wataalamu tunafurahi sana pale wakulima wanapotuita ili tuwaelekeze njia bora za kilimo kwa ajili ya manufaa yao wenyewe kwani sie tupo kwa aajili yao na tumeajiriwa na serikali ili tuwatumikie wao". Pia ametoa wito kwa wakulima kufika kituoni hapo ili waweze kujifunza mengi kuhusu kilimo kwani wakifika mahali hapo waweza kujifunza hata kimatendo na mwisho wa siku kupata manufaa katika kilimo. "Tunataka kuwa na Tanzania yenye wakulima wanaojua nini wanafanya katika kazi zao, kwani kilimo chenye manufaaa bado hakijafanikiwa Tanzania, tunatamani sana tena sana"
Hata hivyo bi Rose alisema japokuwa kuna changamoto ya kuwa na mbegu feki madukani kitu ambacho kinasababisha wakulima kutokuwa na imani na mbegu za madukani, lakini amewahakikishia wakulima kuwa wanauhakika na mbegu wanazozalisha kituoni hapo.
hivyo amewaasa wakulima kuwa waangalifi wanapokwenda madukani kwa kuzitambua nembo halisi katika pakiti za mbegu wanazonunua.
Shamba la ngano
Maharage yaliwa tayari kwa kuvunwa
Kituo hiki ambacho kipo mkoani mbeya kimekuwa kikifanya utafiti wa mazao mbalimbali ili kupata mbegu bora kwa ajili ya wakulima. Na pia wamekuwa wakifanya utafiti wa udongo pamoja na magonjwa kwa mimea ili kumuondoa mkulima kutoka kwenye kilimo cha kupata chakula tuu bali wanataka mkulima apate hata mazao ya ziada ili kupata faida zaidi kwa kuyauza mazao hayo.
Bi Rose akichunguza aina ya ugonjwa kwa kutumia darubini
Bi Benadetha Rugumisa yeye ni biotechnology kituoni hapo
Akieleza kuhusu changamoto wanazozipata wakulima Bi Rose amesema kuwa wakulima wamekuwa wakiweka mambo ya imani mbaya hata katika kilimo kitu ambacho amekikemea vikali na badala yake amewasihi wakulima kutofuata maneno ya watu bali wafuate kanuni ambazo wataalamu wa kilimo wamekuwa wakiwafundisha. Ametoa mfano wa wakulima kutoamini juu ya mbegu zinazouzwa madukani kwa kusema kuwa si mbegu nzuri kwa afya za binadamu eti kwasababu tu zimeboreshwa, na badala yake Bi Rose amesema kuwa wao ni watanzania halisi na hawawezi wakafanya kitu kibaya kwa watanzania. Pia amesema hawawezi kutengeneza mbegu mbaya kwani hata wao ni watumiaji wa mbegu hizi hivyo wako makini saana katiaka kutafiti mbegu hizo. Hata hivyo amewasihi sana kutumia mbegu bora zinazouzwa madukani na kuachana na imani mbaya ambayo imewaacha wakulima wengi kuingia hasara kila wanapolima mazao na kuzidi kubaki katiak maisha duni siku zote.
Akifafanua kuhusu uboreshaji wa mbegu alisema kuwa mbegu zilizoboreshwa ni zile zilizochanganywa sifa za mbegu mbalimbali katika mbegu moja ambayo ndiyo iliyoboreshwa kwa kuziunganisha halisia zake {cross}. Na uboreshaji wa mbegu hufanyika kwa njia halisi bila kuongeza kitu kingine chochote ndani yake.
Akiongea kuhusu maharage, Rose amesema kuwa msimu huu wa kilimo uliopita wametafuta sample ya majani ya magonjwa mbalimbali kutoka kila mahali ili kutambua magonjwa shambulizi ya maharage ili waweze kugundua magonjwa sumbufu na mwisho wa siku waweze kudhibiti magonjwa hayo kwa kuzalisha mbegu stahimilivu wa magonjwa hayo ama kwa kutafiti dawa ambayo itadhibiti magonjwa hayo.
Mwisho amewasihi wakulima kutumia maonyesho ya wakulima yajulikanayo kama nane nane amabay hufanyika kila mwezi August {8} kwa manufaa zaidi kwa kuwauliza wataalamu wa kilimo maswali yenye manufaa na kutaka kujifunza kutoka kwao hata kimatendo baddala ya kuyatumia maonyesho hayo kwa kujifurahisha. Amewasihi sana kutembelea Banda la kilimo nanenane mkoani Mbeya na wao wako tayali kwa moyo mkunjuf ili kuwasaidia wakulima, na baada ya maonyesho pia waweze kufika kituoni uyole kwa msaada zaidi. Pia ametoa wito kwa vyomba vya habari kuwaunga mkono wataalamu wa kilimo kote nchini kuwaelimisha wananchi njia ya kilimo bora na matumizi ya mbegu bora.
No comments:
Post a Comment