Pages

Translate

Thursday, 4 July 2013

UWOYA AJA NA MPYA

  AJICHORA MAKANYAGIO YA MWANAE MGOGONI


Staa  wa muvi za Bongo, Irene Pancras Uwoya ameonesha upendo wake kwa mwanaye Krrish Ndikumana kwa kujichora ‘tatuu’ mgongoni yenye nyayo (makanyagio) ya mtoto huyo na kuzisindikiza na jina lake kwa juu.

Baada ya mchoro huo kukamilika, Uwoya aliitumbukiza kwenye mtandao wake wa kijamiii wa Facebook na kutazamwa na watu kibao ambao waliipenda.

Hata hivyo, baadhi ya watu waliozungumza na mwandishi  wetu kuhusiana na tatuu hiyo walisema Uwoya amefuata nyayo za wanawake wengi wa Kiafrika ambao wakishazaa huwapenda sana watoto kuliko baba zao.
 

“Picha ni nzuri, mama ameonesha upendo wake kwa mtoto lakini hii ni tabia ya wanawake wengi wa Kiafrika, wakishazaa mapenzi yote wanayahamishia kwa watoto badala ya waume zao.
 


“We fuatilia utagundua ndoa nyingi huanza kuyumba baada ya mke kujifungua, maana mapenzi yote yanahamia kwa mtoto, mume kama hana subira anaanza kutafuta mwanamke mwingine wa kumpenda upya.


No comments:

Post a Comment