Moshi.
Mashahidi wawili wa upande wa mashtaka, wameieleza mahakama namna
wanyamahai, wakiwamo twiga wanne, walivyosafirishwa kwenda Doha nchini
Qatar kwa kutumia ndege ya jeshi.
Mashahidi
hao, akiwamo mmoja wa madereva wa lori, walitoa ushahidi wao juzi
wakiongozwa na jopo la mawakili watatu wa Serikali, Evetha Mushi, Pius
Hilla na Stella Majaliwa.
Shahidi
wa sita, Davis Kimei aliyekuwa dereva wa lori aina ya Mitsubish Fusso,
alieleza namna alivyosafirisha wanyama hao toka Arusha hadi Uwanja wa
Ndege wa Kilimanjaro (Kia).
Mbele
ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Simon Kobelo shahidi huyo alidai Novemba 25,
2010 alikodishwa kubeba wanyama hao na watu watatu, wakiwemo wawili
wenye asili ya kiasia hadi uwanja wa Kia kwa ujira wa Sh150,000.
“Baada
ya kuelewana tulikwenda hadi kwenye nyumba moja eneo la Kwamrefu,
Arusha na humo ndani nilikuta vijana wengi ambao walikuwa wakitengeneza
mabox yaliyokuwa na Twiga na Swala,” alisema.
Shahidi
huyo alidai baada ya kuwapakia wanyama hao, msafara wa malori manne
ulielekea Kia na kufika saa 8:00 usiku na kuelekea moja kwa moja
uwanjani ambapo walikuta ndege kubwa ya jeshi imeegeshwa.
“Maboksi yale yalishushwa na kupakiwa katika ndege hiyo usiku ule wa manane,” alisema.
Shahidi
wa saba, alidai siku ya tukio saa 4:00 usiku aliwasikia wafanyakazi
wawili uwanjani hapo, wakisema kuna wanyama wangesafirishwa usiku huo.
“Nilimdokeza
mkuu wa upelelezi… Nilipokuwa nyumbani bosi wangu alinipigia simu na
kuniambia ile taarifa niliyompa ilikuwa ni ya kweli kuna ndege ya
Serikali inasafirisha wanyamapori,” alisema.
Shahidi
huyo alidai kuwa saa 6:00 usiku alirudi kazini na ilipofika saa 8:30
usiku lilikuja basi aina ya Toyota Coaster ambapo walishuka watu wenye
sare za jeshi wenye asili ya kiarabu.
Washtakiwa
katika kesi hiyo inayovuta hisia za Watanzania wengi ni Kamran Ahmed,
Hawa Mang’unyuka, Michael Mrutu na Patrick Paul na kesi hiyo itaendelea
kusikilizwa Agosti 13 na 14.
No comments:
Post a Comment