Diamond alisema kuwa yamekuwepo maneno ya chinichini kuwa ameshatoa mahari na siku si nyingi ataingia kwenye maisha ya ndoa ila ukweli ni kwamba kila kitu kinafanyika kwa umakini na mashabiki watajulishwa hatua kwa hatua.
“Suala la ndoa yangu nalifanya kwa umakini sana, watu wawe na subira tu ila wanachotakiwa kujua ni kwamba nina plani za kuifanya sherehe ya ndoa yangu kwenye Uwanja wa Leaders Club, pale Kinondoni na watu wataingia kwa kiingilio kisichopungua shilingi elfu kumi. Itakuwa ni ndoa ya Wasafi bana,” alisema Diamond
chanzo:globalpublishers
No comments:
Post a Comment