Pages

Translate

Friday, 21 June 2013

SPIKA ANNA MAKINDA, EDWARD LOWASSA WAHUSISHWA KUPINGWA KWA MBUNGE.


 
WAZIRI Mkuu aliyejiuzuru Edward Lowassa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya wa Tanzania Anne Makinda wametajwa kuhusika katika tukio la kupigwa kwa Mbunge wa Arumeru Mashariki (Chadema), Joshua Nassari.

Nassari ambaye alipigwa na watu aliowaita kuwa ni wanachama wa CCM Juni 16 mwaka huu kwenye vurugu za uchaguzi mdogo wa udiwani Kata ya Makuyuni Wilayani Mond
uli Mkoani Arusha alisema Makinda hampendi tangu alipoingia Bungeni.

Akizungumza na Habarimpya.com akiwa kwenye chumba alicholazwa katika Taasisi ya Tiba ya Magonjwa ya Mifupa na Ufahamu Muhimbili (Moi), Nassari alidai Lowassa anamchukia tangu alipomshinda mkwewe Sioi Sumari, kwenye uchaguzi mdogo wa ubunge uliofanyika Aprili mwaka jana.
Nassari aliyekuwa amelazwa katika Hospitali ya Selian ya jijini Arusha kabla ya kuhamishiwa MOI, alidai kupigwa na kuchaniwa nguo na Green Guard wa CCM wakati alipokuwa katika jitihada zake za kuhesabu kura kwenye uchaguzi wa udiwani wa Kata ya Makuyuni-Monduli.

“Kipigo nilichopata Lowassa anahusika ananichukia, anataka urais lakini hawezi kuupata kwa kuuumiza watu kama hivi, alifikiri kwamba nitakufa sitakufa hadi kwa mapenzi ya Mungu, Makinda naye ananichukia na hapendi hata kuniona Bungeni” alisema, Nassari.

Alisema kuna jambo ambalo wananchi wanapaswa kulifikiria ni jinsi ambavyo kumekuwa na matukio ya kutekwa na kuvamiwa, lakini hakuna yanayohusisha kiongozi wa CCM, badala yake ni raia wa kawaida na viongozi wa dini na siasa. 

Nassari alidai akiwa kama wakala mkuu wa Chadema katika kata hiyo, alikumbana na mambo kadhaa yaliyomshangaza, ikiwa ni pamoja na kufanyiwa jaribio la kutekwa mara mbili, kabla ya kushambuliwa kwa kipigo.

No comments:

Post a Comment