
Maajabu  ya  uumbaji  yamemfanya  mama  mzazi  wa  Xiao Wei  ambaye  ni  mchina amwage  machozi  akiomba  msaada  wa  kunusuru  maisha  ya  mwanae   mwenye  umri  wa  miezi  7 aliyezaliwa  na  kitu kama mkia
Kitu hicho mathalani  kama  mkia  mfupi, wenye  urefu  wa   sentimita  8  ( 8 cm ), katikati  ya  makalio  mengine  mawili. 

Akiongea   kwa  uchungu, mama  mzazi  wa  mtoto  huyo  amedai  kuwa  kwa  muda  mrefu  amekuwa  akiwaomba  madaktari  wafanye  upasuaji  wa  mkia  huo  lakini  wao  wamekuwa  wakimjibu   kuwa  hiyo  si  kazi  nyepesi  kama  anavyodhani 

"Tukilikata  litaota  tena, hivyo  hatutakiwi  kukurupuka  na  badala  yake  tutakiwa  kupata  muda  wa  kupitia  vitu  vingi  ukiwemo  mrija  wa  uti  wa  mgongo  ambapo  mkia huo umejitenganisha na makalio yake" .Alisema  daktari  mmoja  akimjibu  mama  huyo
 
 
No comments:
Post a Comment