Pages

Translate

Saturday 22 June 2013

KAULI YA PINDA INAZALISHA VIJIMAMBO KILA KUKICHA


PINDA KAWAPA WANANCHI HAKI YA KUJITETEA DHIDI YA POLISI?


        Kwa mara nyingine tena Waziri Mkuu Pinda ametoa kauli ambayo inatafsirika kuwa ni kuhalalisha vyombo vya usalama kuvunja haki za msingi za wananchi kwa kuwapiga na hata kuwaua. Kauli hiyo iliyotolewa wakati wa kujibu maswali Bungeni inatukumbusha sisi wengine kauli yake nyingine aliyoitoa wakati mauaji ya Albino yamepamba moto pale alipoonekana kuhalalisha wananchi kuchukua hatua mikononi. Inawezekana watu wengi wameshasahau kauli ile. Akizungumza Bungeni Waziri Mkuu Pinda akionesha kuchoshwa na mauaji ya Albino alisema hivi “Mkimuona mtu akamkata mwingine shingo naye muueni kwani sasa viongozi wote tumechoka... no more, I can't tolerate anymore (imetosha, siwezi kuvumilia tena” na hakuishia hapo bali aliagiza Umoja wa Vijana wa Chama chake kutekeleza agizo hilo kwa kuwaambia “Umoja wa vijana wa CCM mna jeshi zuri ambalo naamini mkiamua mnaweza kutokomeza mauaji ya wazee wetu pmoja na ndugu zetu maalbno na kazi hiyo nawaagiza muanze leo msisubri auawe mwingine tena”

       Kitu ambacho Pinda hajakielewa na inaonekana hana uwezo wa kukielewa ni kuwa hakuna binadamu anayependa kutendewa kama vile si binadamu. Hakuna mwanadamu ambaye anaweza kuendelea kukubali kudharauliwa, kupuuzwa, kunyanyaswa na kuteswa kwa vile tu wale wanaofanya hivyo wanaamini wanauwezo wa kufanya hivyo. Kauli ya Pinda ni ushahidi wa yeye na wale walioshangilia kutokujua historia.

 

      Nimesoma baadhi ya michango ya watu ambao wanaunga mkono kauli ya kipuuzi kama hii wakiamini wanafanya hivyo wakiwakilisha jambo jema. Historia inao watu kama hao na ni wengi wameenda na kusahauliwa katika giza la historia wakiamini walikuwa wanatetea ‘uzalengo’ au ‘utaifa’. Ni vizuri kumkumbusha Pinda na mashabiki wake kuwa binadamu ana kikomo cha kunyanyaswa, kupuuzwa na kudharauliwa anapofika kwenye kikomo hicho (prespice) mwanadamu atachukua hatua tu!

No comments:

Post a Comment