Pages

Translate

Sunday 23 June 2013

BIASHARA YA MADAWA YA KULEVYA YAPAMBA MOTO

Raia 2 wa Nigeria wakamatwa na SEMBE(Madwa ya kulevya)nchini Kenya
Wawili hao waliokuwa wanaelekea nchini Nigeria kutoka Brazil, walikuwa wamemeza vidonge 54 vyenye Cocain lakini baada ya kuwekwa chini ya uchunguzi wa polisi wakaweza kuvitoa vidonge hivyo.
Wawili hao walikamatwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta mjini Nairobi wakitoa Brazil kuelekea mjini Lagos, Nigeria.
Asubuhi ya leo walipelekwa katika mahakama moja mjini Nairobi na kushtakiwa kwa kosa la kumiliki madawa ya kulevya ambayo ni haramu nchini Kenya.
Ni wiki hii tu ambapo mzozo wa kidiplomasia umekuwa ukitokota kati ya Nigeria na Kenya baada ya kufurushwa kutoka nchini humo kwa mfanyabiashara mwenye utata raia wa Nigeria Anthony Chinedu baada ya kuhusishwa na biashara haramu ya madawa ya kulevya.

Chinedu alirejeshwa Nigeria kufuatia amri ya rais wa nchi hiyo Uhuru Kenyatta kuwa raia wa kigeni wanaohusika na biashara haramu za madawa ya kulevya wurejeshwe kwao.
Hata hivyo mzozo ulianza pale ndege ya Kenya iliyokuwa imewabeba maafisa wa Kenya waliokuwa wanamrejesha Chinedu nchini Nigeria ilipozuiliwa katika uwanja wa Ndege wa Murtallah baada ya kumfikisha Chinedu nyumbani.
Kwa sasa juhudi za kidiploamsia zinagli zinaendelea kuweza kuwarejesha Kenya maafisa hao. Maafisa wa Nigeria wamezungumzia mzozo huo wakikanusha madai kuwa maafisa wa Kenya waliteswa

No comments:

Post a Comment