ASKARI POLISI WAJIPANGA KUHARIBU BIASHARA YA MAKAHABA WAKATI WA ZIARA YA RAIS WA MAREKANI BARACK OBAMA.
WAKATI wafanyabiasha ya ukahaba jijini Dar es
Salaam wakijipanga kutekeleza kauli ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
kimataifa Bernard Membe, yakuwataka watanzania kuchangamkia biashara zao
na kutokubali wageni warudi na dola makwao, Jeshi la polisi limejipanga
kuwadhibiti.
Wakizungumza na habarimpya.com makahaba hao waliokuwa wamejipanga kujipatia
pesa za kigeni kutoka kwa baadhi ya wageni ambao wangewahitaji, walisema Askari
Polisi wamejipanga kuvuruga biashara zao.
Hatua ya Jeshi
la Polisi kuendelea kuwasaka makahaba hao imezidi kuvuruga mipango yao ya
kupata dola chap chap, oparesheni ina yozidi kufanyika hasa maeneo ya Kinondoni,
pengine ikabunguza dola chap chap kama alivyo agiza Membe.
“Kwa kweli mpaka sasa hatujaelewa itakuwa vipi kwani ni kitu cha ajabu
sana na imekuwa tofauti na matarajio tuliyokuwa
tumejiwekea,mwanzoni tuliifurahia sana kauli ya waziri Membe
iliyosema,watanzania tuchangamkie biashara zetu, tusizubae wageni warudi na dola
zao kwao sasa naona imekuwa kinyume kwani ulinzi uliopo ni balaa” alisema mmoja
wa makahaba aliyejitambulisha kwa jina la Zamda aliyesafiri kutoka Dodoma kuja
jijini Dar es Salaam.
Mbali na Makahaba, wamachinga pia wameonekana kukosa maeneo ya kufanyia
biashara zao katika maeneo mabalimbali ya jiji, baada ya Polisi kuongoza
oparesheni hiyo inayoendelea sehemu mbalimbali za jiji hilo.
Akizungumza na Habarimpya.com Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni
Camillus Wambura alisema, “Tumeamua kuimarisha ulinzi wa Jiji na
kuliweka safi jiji letu, sio kwa ajili ya ujio wa Rais Obama tu, bali hii
oparesheni mpya itakayo endelea kufanyika ndani ya jiji hili hata wageni
hawa pindi watakapo ondoka, tumeamua kuifanya Kinondoni kuwa mpya kwa kuzuia
mambo yote yanayotendeka kinyume cha sheria”.
No comments:
Post a Comment