Hatua kwa hatua chini ya ulinzi mkali wa askari shupavu.
|
Askari
akiwa amemnasa mahabusu aliye kimbia mara baada ya kujipaka kinyesi
katika mahabusu ya mahakama ya wilaya ya Nyamagana na Mahakama ya
Mwanza. NA MATUKIO NA VIJANA |
Baada
ya kumkamata na kumrejesha katika chumba cha mahabusu mahakamani hapo,
kwanza mtuhumiwa huyo aliamriwa kuzoa mtondoro wa kinyesi cha binadamu
alichokuwa amejimwagia na kutapakaa chini na mara baada ya kumaliza
kuzoa uchafu huo, alipelekwa kwa hakimu ambapo alisomewa kosa la kula
njama za kutoroka na kukumbana na adhabu nyingine ya kuhukumiwa kifungo
cha miezi sita (6) jela, huku kesi yake iliyokuwa ikimkabili awali
ikiahirishwa.
|
"Kama alivyojipaka ndivyo alivyo yazoa..." |
|
Moja baada ya jingine. |
|
Hatua kwa hatua chini ya ulinzi mkali wa askari shupavu. |
|
Huku
akiweka kinyesi hicho kwenye ndoo mahabusu huyo alilazimika kukizoa kwa
mikono kama muuza mkaa apimavyo mkaa kwenye kopo kuwauzia wateja wake. |
|
Mchafuzi wa mazingira akiadabishwa kabla ya kwenda kusomewa kesi nyingine ya kula njama za kutaka kutoroka. |
|
Hatari....Mahabusu mmoja
aliyekuwa mahabusu ya mahakama ya wilaya ya Nyamagana na Mahakama ya
Mwanzo iliyopo eneo la jirani na Mamlaka ya maji safi na Hifadhi ya
Mazingira (MWAUWASA) jijini Mwanza alitoa vioja vya mwaka kwa kujaribu
kutoroka kwa kujipaka kinyesi ili asiguswe wala kukamatwa.
Mtuhumiwa
huyo ambaye jina lake halikufahamika alijimwagia kinyesi kilichokuwa
kwenye ndoo iliyokuwa ndani ya sero ya Mahakamani hapo na askari
alipokwenda kufungua ili kuwapeleka watuhumiwa kwenye chumba cha
Mahakama kusomewa kesi yake baada ya kutajwa na karani wa Mahakama ya
mwanzo, baada ya kutajwa ndipo mahabusu huyo alipopata mwanya wa
kukimbia na kutoa tahadhari kwa atakaye mgusa au kumshika atakumbana na
kadhia ya kuchafuliwa kwa kupakwa kinyesi. Askari mwingine mwenye
cheo cha sajenti, ambaye alikuwa akihushughulika na huduma nyingine
mahakamani hapo, kwa kuwa alikuwa na uzoefu wa kupambana na mikasa na
vioja kama hivyo vya mahabusu wanao kula njama za kutaka kutoroka
aliamua kula naye sahani moja kwa kumkimbiza na kufanikiwa kumkamata. |
No comments:
Post a Comment