MTOTO wa kike mwenye umri wa miaka mitatu, Maryment Ibrahim ambaye anaishi Tandale jijini Dar es Salaam, hivi karibuni alipatwa na masahibu makubwa baada ya kutekwa nyara na kutoroshwa hadi Gairo mkoani Morogoro huku mtekaji akidaiwa kutaka apewe shilingi milioni 6 ili amuachie.
Mama mzazi wa mtoto aliyetekwa akiwa na mwanaye.
Tukio
hilo la kusikitisha lilitokea Oktoba 16 mwaka huu baada ya kijana
mmoja, anayefanya biashara ya kuuza chipsi anayejulikana kwa jina la
Issa Ramadhani, kudaiwa kumchukua mtoto huyo aliyekuwa akicheza
nyumbani kwao na kutoweka naye kabla ya wazazi wake kubaini na kwenda
kutoa taarifa kituo cha Polisi Kijitonyama ‘Mabatini’.Awali, ilidaiwa Ramadhan alikuwa na tabia ya kuwachukua watoto wadogo wa mtaani hapo na kuondoka nao na kuwarudisha baadaye, kitu kilichowafanya wazazi wa mtoto huyo kutokuwa na wasiwasi.
Mtuhumiwa wa utekaji.
Wakizungumza
na mwandishi wetu, wazazi wa mtoto huyo walisema waliamua kutoa taarifa
polisi na kufunguliwa jalada nambari KJM/RB/8994/13 baada ya kupashwa
kuwa mtekaji ambaye alishaacha kazi yake ya kukaanga chipsi, aliondoka
muda mrefu na binti yao na hakukuwa na dalili za kurejea.Baada ya kuhangaika kwa muda mrefu, wazazi hao pamoja na majirani walifanya uchunguzi wa chinichini na kufanikiwa kupata namba ya simu ya mtekaji huyo, lakini walifanikiwa kubadilishana naye ujumbe mfupi wa simu kwani hakuwa akipokea simu yake ya kiganjani.
Baba mzazi wa mtoto aliyetekwa akiwa na mwanaye.
Inadaiwa
kuwa katika mawasiliano hayo, mtekaji alikataa katakata ombi la kumtaka
amrudishe mtoto wao na kutaka apewe kiasi cha shilingi milioni 6 ili
kutekeleza jambo hilo ingawa baadaye ilibainika jamaa huyo alikuwa
Gairo mkoani Morogoro.
Mtoto Maryment Ibrahim aliyetekwa na Ramadhan.
Wazazi
hao walisema kuwa Oktoba 19 mwaka huu mmoja wa majirani walioguswa na
tukio hilo aliyejitambulisha kwa jina la Justin Henry alijitolea
kusafiri mpaka Gairo kumsaka mtoto na mtekaji wake jambo ambalo
lilifanikiwa kwa kumpata mtoto akiwa mzima wa afya japokuwa mtekaji
alishtukia na kukimbia.
No comments:
Post a Comment