Pages

Translate

Wednesday, 18 September 2013

TaCRI NA HRNS ZIMEFANYA KAZI YAKE, KAZI KWAO WAKULIMA.




 
Taasisi ya Utafiti wa Kahawa Tanzania (TaCRI) iliyopo mkoani Kilimanjaro ilianza kazi rasmi 2001 na imepata mafanikio makubwa katika utafiti wa mbegu mpya chotara za arabika pamoja na ile ya Robusta
 Aina hizi za miche bora chotara za kahawa zimekuwa ni mkombozi mkubwa katika sekta ya kahawa kwa kuwa zina tija ya hali ya juu zaidi ya aina za zamani pia zina muonjo wa hali ya juu kama aina za zamani na hata zaidi, na zina ukinzani na magojwa hatari ya chulebuni (CBD), kutu ya majani (CLR) na mnyauko fuzari (CWD), (CBD) kutegemea aina ya kahawa

 Kutokana na sifa hizo, aina hizo mpya zinampunguzia mkulima gharama za uzalishaji, kati ya asilimia 50 na hata ukilinganisha na miche mingi ya zamani ambayo mingi imezeeka na kushambuliwa na magojwa kitu ambacho kinasababisa hasara kwa mkulima 

Pia TaCRI imetoa teknolojia za kuongeza tija na ubora wa kahawa aina mbili zinazotekelezeka za kuzalisha miche mipya bora ya aina hizi chotara ikiwa nipamoja na kutumia vikonyo, kupachika aina mpya juu ya mibuni ya zamani na kuzalisha kitaalamu miche kwa kutumia chupa ikifahamika kwa lugha ya kingereza ’Tissue culture au Somatic embryogenisis.’

Taasisi hii ikiwa ndio uti wa mgongo katika sekta ya kahawa na sasa imefanikiwa kutoa teknolojia mpya ya kuongeza tija na ubora wa kahawa nchini kwa msaada mkubwa wa nchi za Ulaya pamoja na fedha kidogo inayopata kutoka kwenye mgawanyo wa bajeti ya serikali ya Tanzania kupitia wizara ya kilimo na chakula.
Ikiwa bado TaCRI imejipanga kufanya mambo makubwa katika sekta hii na kuikomboa Tanzania kiuchumi kwani kwa sasa kahawa inachangia asilimia 22 ya pato la Tanzania, serikali pia inatakiwa kuunga mkono kazi zinazofanywa na TaCRI kwa kuwekeza zaidi katika utafiti ili kupunguza makali ya kazi na kumuelemea mkulima atakapo kununua miche kutoka kwenye taasisi hiyo na hata kuiwezesha taasisi hiyo kifikia malengo kwa kuzalisha idadi kubwa ya miche chotara na kukikomboa kilimo cha kahawa Tanzania.

Akiongea na waandishi wa habari waliotembelae taasisi hiyo chini ya Bioscience For Farming in Africa (B4FA) ili  kuona uhalisia wa utafiti unavyokwenda mmoja wa watafiti ambaye hakupenda jina lake litajwe asisema kuwa “hapo awali serikali ilitoa pesa za kutosha kwa ajili ya utafiti wa miche hiyo na walifanya kwa nguvu kubwa na mafanikio, lakini kwa sasa bajeti waipatayo kutoka  wizarani ni kidogo sana kiasi ambacho hakilingani kabisa na kazi tunayoifanya hapa, kwa mfano mwaka wa bajeti wa 2013/14 taasisi yetu imetengewa shilingi milioni mia moja ambayo ni kiasi kidogo sana kwa taasisi kama hii” alisema mtafiti huyo
Kwa kiwango ambacho kimefikiwa na TaCRI ni mafanikio makubwa katika tasnia hii ya kilimo na kubakia kazi kwa mkulima kuitikia wito kwa kuanza kupada miche bora au kupandikiza vikonyo kwenye miche ya zamani ili kuwa na kilimo chenye tija.

Ikiwa TaCRI wao wamejizatiti katika utafiti wa miche bora taasisi isiyo ya kiserikali ya Hanns R. Neumann Stiftung Tanzania (HRNS) ambayo pia ipo mjini Moshi mkoani Kilimanjaro wao wamejito kuwaunga mkono wakulima wa kahawa kwa kutoa elimu ya kilimo cha kahawa hasa matuzi ya miche bora. Hivyo kwa kushirikiana na TaCRI katika kuhamasisha matumizi ya miche ya kahawa iliyoboreshwa wamewaunganisha wakulima katika vikundi na kuwawezesha wakulima kuanzisha bustani za miche ya kahawa ili kurahisisha upatikanaji wa miche hiyo.

HRNS wamekuwa watoaji elimu hii kwa vitendo kitu ambacho kimewasaidia wakulima wengi kuanza kulima kahawa upya kitu ambacho kilikuwa hakipo kutokana na wakulima wengi kukata tamaa kwa kuona kuwa kilimo cha kahawa ni cha hasara kutoka na miche ya zamani kuzeeka na kushambuliwa na magonjwa hivyo kutozaa matunda.

“Tumekuwa na mashamba darasa ambayo wakulima wengine wakiona matokea ya shamba huhamasika na wao kulima kahawa, pia tumekuwa tukitembelea vikundi na mashammba ya wakulima ili kuwashauli na kuona maendeleo ya mashamba yao  ” alisema bwana Tadeus Moshiro ambaye ni meneja wa mradia wa HRNS

“Na kazi hizi tunafanya na mikoa yote inayolima kahawa bila kijali ni aina gani ya kahawa, na tumepata mafanikio makubwa sana mkoani Mbeya ambapo mwitikio wa wakulima ni mkubwa sana na mikoa mingine pia tunaona mwitikio huo japo wakulima wengi hulalamika bei kubwa ya bembejeo za kilimo” Tadeus alisema

Kutokana na pembejeo za kilimo kuwa juu wakulima wengi wamekuwa wanashindwa kumudu kilimo cha kahawa hivyo taasisi hii ya HRNS huwaunganisha wakulima wa kahawa ili waweze kupata mikopo katika mabenki yanayotoa mikopo kwa mkulima ili waweze kumudu kilimo na kupata mazao yenye tija kwa mkulima.

Hata hivyo HRNS imekuwa ikiwakujulisha wakulima bei ya kahawa kila mara ili kuwawezesha wakulima kujua hali halisi ya soko la hakawa kwa wakati.

Akizungumza kwa upande wa wakulima Bwana wa Moshi vijijini aliishukuru sana TaCRI kwa elimu waliyompa na kumuwezesha kutoka kwenye kilimo duni mpaka kumfikisha kwenye kilimo chenye tija na kuwa kama mfano wa kuigwa kijijini hapo, kwani ametoka kwenye uzalishaji wa gunia 1la kahawa mpaka kufikia kwenye magunia 6 ya kahawa kutokana na miche bora ya TaCRI.

Pia Bi Magdalena Temba Ambaye ni mtunza hazina wa kikundi cha Zinduka Farmer Group cha Kiruwa, Moshi ameshukuru HRNS kwa elimu waliyowapa na kuwawezesha wao kama kikundi kuwa na bustani yao ya miche bora ya kahawa ambayo huiuza kwa wakulima wenzao na kuwapatia kipato na kumuwezeza kila mwana kikundi kuwa na shamba lenye miche bora kitu ambacho si rahisi kwa mkulima mmoja mmoja kufanya hivyo kirahisi. Pia amewataka wakulima wa kahawa kote nchini kubadirisha miche ya kahawa kwa kupanda miche mipya iliyobora ama kupandikiza miche bora juu ya kikonyo cha kahawa ya zamani ili kupata faida zaidi katika kilimo. Na kushauri wakulima kujiunga katika vikundi ili kujikwamua kimaendeleo kwa kushirikiana na wakulima wengine

Licha ya bei ya kahawa kuwa chini na kuwafanya wakulima wengi kukata tama ya kuendelea na kilimo hicho na kufanya wakulima wengi kuanza kulima mazao mengine kama maharage, ndizi na mahindi, Bwana Tadeus Moshiro amewasihi wakulima kupanda miche mipya ya kahawa kwani inakuwa haraka na huchukua mda mfupi kuanza kutoa matunda ambapo nikipindi cha mwaka mpaka mwaka na nusu kuanza kuzaa. Na kwakufanya hivyo itamuwezesha mkulima kupata mazao mengi na yenye ubora wa juu hivyo kumuwezesha mkulima kuuza kahawa kwa bei nzuri zaidi yenye faida kwake na Taifa pia

Mbali na hayo yote wakulima wa kahawa mkoani Kilimanjaro wameiomba serikali ya Tanzania kuwa, kauli ya kilimo kwanza isiwe kwenye mahindi na mazao mengine ya chakula kwa kutoa ruzuku za pembejeo kwenye mazao hayo tuu bali kilimo kwanza itumike mpaka kwenye mazao ya biashara kama kahawa.
Hata hivyo kazi imebaki kwa mkulima kuitikia wito wa TaCRI  pamoja HRNS  kulima kahawa kwa kutumia miche mipya ya kahawa ili kujitoa kwenye kilimokisicho na tija na kulima kwa tija ili kujiongezea kipato cha mkulima mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.



1 comment: