Sister feki baada ya kunaswa akikusanya fedha.
Akipekuliwa mabegi yake nyumbani alipokuwa akiishi.
POLISI mjini Narok nchini Kenya
wanamshikiria mwanamke mmoja aliyenaswa akiwa na mavazi ya kitawa
akikusanya fedha kutoka kwa watu wenye mapenzi mema akidanganya kuwa ni
sister. Mwanamke huyo alikuwa akikusanya misaada ili aweze kurudi katika
konventi alipotokea mpaka hapo aliposhutukiwa kuwa hakuwa mtawa.
Alipopekuliwa nyumbani kwake alikutwa na vitambulisho kadhaa. Mpaka
ananaswa, sister huyo alikuwa amewatapeli watu kadhaa na anatarajiwa
kufikishwa mbele ya sheria kesho.
No comments:
Post a Comment