Pages

Translate

Monday 2 September 2013

SAKATA LA MADAWA YA KULEVYA,DIAMOND APOKONYWA PASSPORT...

 
 Ni mwendelezo wa Sakata la unga ambalo sasa ni janga kwa taifa letu. Orodha zinaendelea kutoka na kuwekwa wazi huku bunge likivutana kuhusu sakata hilo. Kila kuitwapo leo waanzania wamekuwa na hamu ya kujua ni nani wahusika wakubwa wa biashara haramu hiyo abapo mpaka sasa watu kathaa wamekamatwa na wengine kuachishwa kazi wakisemekana kufanya kazi hiyo.

Tetesi za kutoka ndani zinasema msanii wa muziki Naseeb Abdul au Diamond ambaye alijitapa wazi mbele ya kamera za habari kuwa anamiliki pesa zaidi ya bilioni moja kwenye akaunti yake, nyumba 5 za thamani Kijitonyama na Mikocheni na anatumia simu 6 za thamani ambazo zipo hewani muda wote tayari amenyang’anywa hati yake ya kusafiria na baadhi ya simu zake katika mwendelezo wa uchunguzi juu yake unaofanywa na vyombo vya dola
Msanii pia wa maigizo Masanja Mkandamizaji ambaye anadaiwa kumiliki mkwanja mrefu na nyumba za thamani kubwa mpaka magari naye tayari ametajwa kuhusika na madawa ya kulevya

No comments:

Post a Comment