Penny,Lulu na Wema enzi za mahusiano yao.
Mtangazaji
nyota nchini ambae ni mchumba wa kupika na kupakua wa mwanamuziki Diamond Penny
amevunja ukimya na kutoa onyo kali kwa wasanii wa kike na wasio wasanii kumlaia
mbali baby boy wake Diamond.
Habari za
uhakika toka kwa mtu wa karibu na Penny anaeishi nae maeneo ya Mwananyamala
ambae pia aliomba hifadhi ya jina lake alisema “ Jamani Penny amejipanga
kuolewa na Diamond kwani sasa hivi amecharuka na kutoa onyo kali kwa mwanamke
yeyote atakae msogelea mchumbaake huyo la sivyo ataroga mtu” Alisema dada huyo
ambae anafanyakazi nyumba ya jirani na anapoishi Penny
Penny
amepiga mkwara huo hasa akimlenga zaidi msanii Lulu na Linah nk huku
akitahadharisha kuwa anawaomba wote wenye tabia ya kuchukua wanaume za
watu kwani yeye katika maisha yake hajawahi kuchukua mume wa mtu hivyo
kama akihisi kuna ajenda yoyote ya siri kati ya mchumbaake na wasanii
hao hakika ataroga mtu kwani yeye ni mtoto Mdigo halisi.
Aidha chanzo
hicho kiliongeza kusema kuwa penzi la Penny na Diamond limefikia pazuri kiasi
cha familia zao kutembelea na kula pamoja kama wakwe. Hata hivyo ilielezwa kuwa
Familia ya Diamond imeshampa Baraka zote mtoto wao ili amuoe kabisa Penny na
huku nae Penny akihimizwa kudumisha upendo wa dhati kwa Diamond ambae tangu
aanze kuishi na mtangazaji huyo Diamond amebadilika sana kitabia kiafya nk.