| 
Habari hii inatokea Nchini Kenya ambapo Msichana mwenye 
umri wa miaka 14  Mwanaharabu Wamukoya kutoka katika 
kijiji cha  Harambee katika wilaya ya Kakamega amejifungua 
watoto watatu wote wakiwa ni Wavulana wawili kati yao
 wamezaliwa wakiwa na uzito wa 1.5 kilogram na mwingine 
akiwa na uzito wa Kilogram 1.3. 
Nesi wa zamu katika Hospitali hiyo ya Bugoma Bi,Mary 
Marumbu alisema Watoto hao pamoja na Mama yao wanaendelea 
vizuri na wakati wowote wanaweza kuluhusiwa kutoka Hospitalini 
hapo. Mshangao zaidi ni pale ilipokuja kujulikana kwamba Baba 
Mzazi wa watoto hao watatu waliozaliwa  bado ni mtoto mdogo 
kama alivyo Mama yao kwani Baba yao ana Umri wa Miaka 16 
ambae pia bado anasoma,Zaidi aliishukuru sana Serikali kwa
 kuweza kuondoa garama kwa wajawazito wakiwa wanajifungua 
na ivyo kuweza  kumuwezesha mzazi mwenzie kujifungua pasipo
 Garama zozote zile. | 
No comments:
Post a Comment