Akizungumza kwa hofu kubwa mama wa mtoto huyo mara baada ya kuulizwa chanzo cha kumfanyia mwanae ukatili huo alisema kuwa alichoshwa na malalamiko ya majirani zake kwa kumtuhumu mwnae kuwa na tabia za wizi wa fedha pamoja na mayai ya kuku.
Baada ya ukatili wa kuunguzwa na maji mama huyo alimfungia mwanae ndani kwa mda wa siku saba mpmka majirani walipo anza kumtafuta bila mafanikio na kuamua kutoa taarifa katika uongozi wa kijiji.
Na ndipo msako mkubwa ulifanyika ulio pelekea kupatikana kwa mtoto huyo aliyekuwa amefungia bila ya kupewa huduma yoyote ya kumtibu mtoto huyo, kitendo ambacho kilipelakea uongozi wa kijiji kutoa taarifa kituo cha polisi Mji mdogo wa Mbalizi.
Mara baada ya kkukamtwa mama huyo alifikishwa katika kituo kikuu mjini Mbeya kwa mahojiano na mtoto Emilly amelazwa katika haspitali aya rufaa mkoani humo.
No comments:
Post a Comment