Binti
wa umri wa miaka 15 tunayemtambulisha kwa jina moja tu la Zaina, mkazi
wa Kimara jijini Dar ameamua kufunguka na kusimulia jinsi alivyokuwa
akibakwa na baba yake mzazi aliyemtaja kwa jina moja la Mohamed. ANAANZA KWA KUANIKA HISTORIA YAKE FUPI! Akisimulia
kwa uchungu, Zaina alianza kwa kuanika historia yake kwa ufupi kwamba
tangu atoke tumboni, hakuwahi kumuona mama yake zaidi ya kuoneshwa
kwenye picha tu! Akasema
hiyo yote ilitokana na hadithi aliyowahi kusimuliwa kwamba, akiwa
kichanga, baba huyo alimuiba kwa mama yake anayeishi Kigamboni, Dar na
kwenda kumlea Kimara kwa ushirikiano na mama yake wa kufikia. Lakini
akasema: Hata huyo mama wa kambo mwaka jana aliachana na baba baada ya
kutufumania chumbani mimi na baba, akakasirika na kuondoka zake.
SIKIA FILAMU KAMILI SASA “Nakumbuka
ilikuwa mwanzoni mwa mwaka jana, nikiwa darasa la tano katika Shule ya
Msingi Kimara ndipo baba alipoanza tabia ya kunilazimisha tufanye
mapenzi. Alisema anataka tufanye kwa njia ya kawaida na ya kinyume na
maumbile.
“Nilikataa
lakini akawa ananilazimisha na vitisho juu. Tulianza kwa kufanya mchezo
huo na baba lakini si kwa kupenda kwangu, nililazimika kwa sababu
niliamini ni baba ambaye anaweza kunifanya lolote kama nitakataa, mbaya
zaidi hakuwa akitumia kinga,” alisema na kuongeza:
“Kuanzia
hapo, zoezi hilo liliendelea kila siku hadi mwishoni mwa mwaka jana
nilipoamua kutoroka na kwenda kuwaeleza ndugu wa baba, kule Tanga.”
Binti
huyo alikwenda mbele zaidi kwa kusema kuwa, kilichomsukuma kutoroka ni
mateso, ukatili na udhalilishwaji uliopitiliza kwani baba yake wakati
akimwingilia alikuwa akimkaba kooni ili asipige kelele. “Yeye
alijua anafanya kosa, akawa akiniingilia huku ananikaba koo nisipige
kelele. Nilikuwa nasikia maumivu makali balaa,” alisema binti huyo.
ALIWAAMBIA MAJIRANI LAKINI WALIOGOPA KUMVAA BABAKE “Kingine
kilichonifanya nitorokee Tanga kuwaambia ndugu zake ni kwamba, niliwahi
kuwaambia majirani kuhusu mchezo wa baba lakini hakuna aliyethubutu
kumuuliza kwa vile wanamuogopa,” alisema.
MAMA MZAA BABA AAMBIWA KILA KITU Zaina alizidi kusema kuwa, baada ya kufika Tanga alimweleza kila kitu bibi yake (mama mzaa baba’ke).
Bibi
huyo kwa sababu ni mzazi alimwita mwanaye na kumkanya kisha akafanyiwa
mambo ya kimila ili kuondoa balaa hilo la baba mtu kutembea na mwanaye
wa kumzaa la sivyo kwa mila za kwao ukoo mzima ungesambaratika.
BABA MTU AONDOKA TANGA USO UMEMSHUKA, YEYE AGOMA “Baada
kufanyiwa mambo ya mila, baba aliniambia turudi Dar lakini nilikataa
kwa sababu niliamini tutakapofika bado atataka kuniingilia tena. Nasema
hivyo kwa sababu pia baba amewahi kufanya mapenzi na dada’angu anaitwa
Hamida mpaka akampa mimba. “Huo
ukatili wote alikuwa akitufanyia kwa nyakati tofauti tofauti, dada
alipopata mimba siku moja alimwibia fedha ili akaitoe, alifanikiwa na
akakimbia nyumbani, sijui alipo,” alisema.
Akaendelea:
Basi, niliamua kubaki kwa bibi, lakini kuna siku alikuja mtu aliyekuwa
anatafuta msichana wa kazi ‘hausigeli’, mimi nikakubali, nikaenda Moshi
ambako nilikaa kwa muda.
“Hivi
karibuni nilirudi Dar na kufikia kwa jirani, sikutaka kwenda nyumbani
kwa baba, namuogopa atataka tena. Huyu jirani niliyefikia kwake, mtoto
wake ni rafiki yangu tulikuwa tunasoma naye. Hapa nilipo natafuta msaada
wa kumpata mama yangu mzazi. Kama atabahatika kulisoma gazeti hili
namuomba anifuate jirani na kwa baba atanipata,” alisema Zainab.
Zainab
hakuishia kwenye kufikia kwa jirani tu, anasema akiwa hapo jirani huyo
kesho yake alimpeleka serikali za mitaa ili kutoa taarifa kuwa amerudi
kwa vile alitafutwa kwa muda mrefu kwenye shule aliyokuwa akisoma.
MWENYEKITI WA MTAA AKIRI ZAINAB KUBAKWA NA BABA’KE Naye
mwenyekiti wa mtaa wa eneo hilo, Demetrius alikiri kumpokea mtoto huyo
na kumsimulia yote kuhusu baba yake ambapo aliambatana naye hadi Kituo
cha Polisi Mbezi kwa Yusuf kwa lengo la kutoa taarifa ili mzee huyo
achukuliwe hatua za kisheria. Alisema binti huyo alifunguliwa jalada la
kesi KMR/RB/114/2013 UCHUNGUZI.
BABA ANASEMAJE? Baada
ya kumalizana na binti huyo aliyeungwa mkono na mwenyekiti huyo,
mapaparazi wetu walizungumza na baba mtuhumiwa ambapo alikuwa na haya ya
kusema:
“Si kweli, huyo mtoto ananisingizia tu, mimi siwezi kufanya kitu kama hicho na binti yangu wa kumzaa hata siku moja.
|
No comments:
Post a Comment