Mwenyekiti wa Umoja
wa Vijana wa CCM(Uvccm) mkoani Arusha, Robinson Meitinyiku amepinga mpango wa
baadhi ya vijana wa jumuiya hiyo wilayani Arumeru kukusanya saini kwa lengo la
kumwondoa mwenyekiti wao. Vijana hao wa Arumeru wakiongozwa na Ally Majeshi
wanakusasanya saini zaidi ya 50 kwa lengo la kumwondoa Mwenyekiti wao,
Boniphace Mungaya kwa madai kwamba hafai. Meitinyiku alisema ofisi yake
imepokea taarifa kuhusu kitendo hicho na tayari imeagiza suala hilo lirudishwe
katika uongozi wa Wilaya ya Arumeru.
No comments:
Post a Comment