Arusha. Polisi wamefanikiwa kumtia mbaroni mfanyabiashara tajiri wa 
madini ya Tanzanite huko Mirerani anayetajwa kuwa ndiye aliyepanga na 
kukodi watu waliomuua bilionea Erasto Msuya.
                                Habari za uhakika kutoka ndani ya Jeshi la Polisi zimedai kuwa mfanyabiashara huyo alikamatwa mwishoni mwa wiki na jana na juzi alikuwa akihojiwa na makachero
Kwa mujibu wa vyanzo hivyo, mfanyabiashara huyo ndiye aliyetoa fedha za 
kununulia pikipiki mbili zilizotumika katika mpango huo na pia alitoa 
fedha kwa ajili ya kununua simu mpya na laini mpya.
                                
“Tumewakamata watu wametupa mwanga mzuri na huyo mfanyabiashara ndiye 
aliyetoa fedha za kununua pikipiki na siku moja kabla ya tukio 
zilihifadhiwa nyumbani kwake,” alidokeza polisi mmoja.
                                
Habari hizo zimedai kuwa polisi pia imewahoji mawakala wa kampuni za 
simu ambao walitumiwa kusajili laini mpya za simu zilizotumika kumpigia 
marehemu na kutumika kupanga mauaji hayo.
                                
Pikipiki hizo mbili, zilinunuliwa siku moja kabla ya tukio zikahifadhiwa
 nyumbani kwa mfanyabiashara huyo hadi siku iliyofuata ambapo 
aliwakabidhi wauaji na zote zimekamatwa.
                                
Mahojiano kati ya mfanyabiashara huyo na Polisi yamekuwa yakifanyika kwa
 siri na katika kituo cha polisi (jina tunalo) na kwamba mambo ni 
mazuri.
 

 
No comments:
Post a Comment