Pages

Translate

Thursday, 22 August 2013

MFANYABIASHARA ALIYEJIREKODI AKIMLAWITI MFANYAKAZI WA DUKANI AKAMATWA



JESHI la Polisi mkoani Kilimanjaro limemkamata mfanyabiashara mashuhuri wa mjini Moshi, Totolii Kimath anayedaiwa kurekodi mkanda wa video ukimwonyesha akimlawiti mfanyakazi wake wa dukani.
 
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Robert Boaz, aliliambia Tanzania Daima kuwa kijana huyo ambaye anamiliki maduka ya kuuza na kutengeneza CD katika kituo kikuu cha mabasi cha mjini Moshi, alikamatwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), akitokea Dubai.
 
Alisema Jeshi la Polisi lilikuwa likifanya uchunguzi kwa muda mrefu wa picha zilizosambaa katika mitandao ya kijamii na simu ambazo zinaonyesha mwanaume na mwanamke wakifanya mapenzi kinyume cha maumbile.
 
“Tulikuwa tunafanya uchunguzi wa picha zilizosambaa kwenye mitandao pamoja na simu kwenye Whatsapp ambazo zinaonyesha watu wakifanya mapenzi kinyume cha maumbile, kimsingi ni kosa la jinai mwanamke kumruhusu mwanaume amuingilie kinyume cha maumbile ama mwanaume amuingilie kinyume na maumbile,” alisema.
 
Alisema bado uchunguzi wa picha hizo unaendelea ikiwa ni pamoja na kumhoji mhusika na kwamba endapo uchunguzi utakamilika atafikishwa mahakamani kwa kosa la kushiriki kufanya mapenzi kinyume cha maumbile.
 
Kifungu namba 154 cha kanuni ya adhabu kimeweka adhabu ya kifungo cha maisha kwa mtu anayepatikana na hatia ya kufanya mapenzi na mtu mwingine kinyume cha maumbile.

 
Video za mfanyabiashara huyo ambazo zimekuwa gumzo zimekuwa zikisambazwa kupitia mitandao ya simu hususan Whatsapp na nyingine zikiuzwa katika maduka yaliyopo stendi kuu ya mabasi Moshi.
 
Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili ulibaini kuuzwa kwa video hizo ambazo zina vipande viwili, kimoja kikiwa na urefu wa dakika 8:47 na kingine dakika 4:00 kwa kiasi cha kati ya sh 3,000 hadi 5,000 katika maeneo mbalimbali ya mji wa Moshi.
 
Inadaiwa kuwa mfanyabiashara huyo kijana anayemiliki maduka matatu Stendi Kuu ya Mabasi, alirekodi video hizo kwa siri bila mfanyakazi wake huyo kujua na kuihifadhi kwenye kompyuta ambazo moja kati ya vipande hivyo inaonyesha akimlawiti mfanyakazi wake huyo.
 
Katika hatua nyingine, taarifa mbalimbali kutoka eneo la stendi kuu ya mabasi zinasema baadhi ya wasichana wanaodaiwa kufanya mapenzi na kijana huyo wameingiwa na hofu kutokana na video nyingine ambazo zinadaiwa kurekodiwa na kijana huyo akifanya mapenzi nao.
 
“Hapa stendi sasa hivi mabinti waliotembea na jamaa wako roho juu maana tayari nimesikia mshikaji alikuwa akirekodi kila msichana aliyetembea naye, sasa wana hofu kuwa video zao pia zitasambaa kama zilivyokuwa hizi nyingine,” alisema kijana mmoja muuzaji wa duka la CD ambaye hakupenda jina lake kutajwa gazetini.

No comments:

Post a Comment