Pages

Translate

Friday, 23 August 2013

HAYA SASA SIJUI TUWAFICHE WAPI WATOTO

Amnajisi mtoto kwa ngono ya mdomoni kwa hadaa ya kumpa mwanasesere

Fundi baiskeli  mmoja mkaazi wa mtaa wa Nsemlwa, wilaya ya Mpanda, mkoa wa Katavi,  Athumani  Mussa (54) amefikishwa jana katika  Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Wilaya ya Mpanda kwa tuhuma za kumlawiti (kunajisi)  mdomoni mtoto msichana (4) baada ya kumdanganya  kumpatia mdoli wa kuchezea.

Mtuhumiwa  alifikishwa  mahakamani hapo na kusomewa mashitaka na mwendesha mashitaka mkaguzi wa msaidizi wa polisi Razalo Masembo mbele ya Hakimu mkazi mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Mpanda Chiganga Ntengwa.

Mwendesha mashitaka aliiambia  mahakama kuwa  mshitakiwa Athumani Musa alitenda kosa hilo Julai 24
mwaka huu majira ya saa 12 jioni nyumbani kwake katika mtaa wa Nsemlwa mjini hapa.

Mtuhumiwa anadaiwa kuwa siku hiyo ya tukio alimwona mtoto huyo akiwa na wenzake wakicheza barabarani karibu na nyumbani kwake ndipo alipomwita mtoto huyo na kumwambia amfuate nyumbani kwake ili akampe mdoli wa kuchezea. Mara baada ya mtoto huyo kuingia ndani, mtuhumiwa alianza kumnajisi mtoto huyo mdomoni huku akiwaamekaa kwenye kochi lake sebuleni.

Ilidaiwa kuwa licha ya mtoto huyo kupiga mayowe ya kuomba msaada, mtuhumiwa hakujali mayowe ya mtoto huyo bali aliendelea na shughuli yake hadi hapo alipomaliza haja yake.

Mwendesha mashitaka alidai kuwa mtoto huyo alipotoka nyumbani kwa mtuhumiwa alielekea nyumbani kwa mama yake huku akilia kwa sauti kubwa, hali iliyosababisha watoto wenzake wamfuate kwa nyuma.

Masembo alieleza mara baada ya kufika kwa mama yake na kuulizwa analia nini, mtoto huyo alitema mdomoni mbele ya mama yake shahawa akimweleza mama yake alichofanyiwa na fundi baiskeli, Musa.

Mama wa mtoto huyo aliangua kilio na kufanya majirani wakusaniyike na ndipo alipowasimulia mkasa huo.

Majirani hao walipochukua jukumu la kwenda kumkamata mtuhumiwa wakiwa wanaongozwa na mtoto huyo ambaye alikataa kuingia ndani ya nyumba ya mtuhumiwa kwa kudai  anaogopa kunajisiwa tena na mtuhumiwa.

Mtuhumiwa Athumani Musa alikana shitaka hilo na Hakimu Mkazi Mfawidhi, Chiganga Ntengwa aliamuru mshitakiwa apelekwe rumande  hadi Septemba 2 kesi yake itakaposikilizwa.

No comments:

Post a Comment