Pages

Translate

Wednesday 17 July 2013

WANASAYANSI NCHINI UINGEREZA WAGUNDUA NJIA YA KUCHAJI SIMU KWA MKOJO


Wanasayansi wa maabara ya Bristol Robotics Uingereza wamegundua njia ya kutumia mkojo kama chanzo cha kuzalisha umeme wa kuchaji betri za simu, na kudai kuwa wa kwanza kutengeneza “the world’s first microbial fuel cells (MFC) powered mobile phone”.

Watafiti hao walielezea juu ya ugunduzi wao kupitia jarida la ‘Physical Chemistry Chemical Physics’.
Dr Ioannis Ieropoulos amesema, huo ndio ugunduzi wa kwanza wa kuzalisha nguvu ya umeme kwa kutumia mkojo, na katika majaribio ya utafiti huo wamefanikiwa kuchaji simu ya Samsung. “By harnessing this power as urine passes through a cascade of MFCs, we have managed to charge a Samsung mobile phone”. Aliongeza “The concept has been tested and it works – it’s now for us to develop and refine the process so that we can develop MFCs to fully charge a battery”.

Wanasayansi hao wanaamini kuwa teknolojia yao inaweza kutumika katika mabafu huko mbeleni kwaajili ya kuwashia mashine za kunyolea au kupasha moto maji ya kuoga na kuwasha taa.

No comments:

Post a Comment