Habari zilizotufikia kutoka mjini
Mtwara Zinasema kuwa Gari lililobeba Shehena ya Mabomba ya Kusafirishia gesi
kutoka Mjini Mtwara kuelekea Dar limeshambuliwa na mawe na kupelekea dereva Wa
lori hilo Kujeruhiwa Vibaya. Lori hilo lilianza kushambuliwa mara baada ya
kuingia katika manispaa ya mikinda Mtwara Mjini Sababu ya kushambulia gari hilo
ni katika kile kinacho dhihirisha kua wana Mtwara bado hawajakubaliana na hoja
ya Serikali ya kutaka Kusafirisha Gesi hiyo kwaajili ya Manufaa ya Nchi.
Lori hilo kwa sasa lipo kituo kikubwa cha polisi Mtwara, Ikiwani wiki moja tu
imepita tokeaa watu kadhaa kukamatwa na jeshi la polisi mkoani Mtwara kwa kile
kinachodaiwa kusambaza waraka wa kuhujumu miundombinuu yote ya gesi mara tu
serikali itakapo anza utekelezaji wake wa ujenzi wa bomba hilo kupeleka Dar.
No comments:
Post a Comment