Pages

Translate

Saturday, 6 July 2013

SH. 500/- SASA ITAKUWA SARAFU BADALA YA NOTI ILI KUIFANYA ISICHAKAE HARAKA

SH. 500/- SASA ITAKUWA SARAFU BADALA YA NOTI ILI KUIFANYA ISICHAKAE HARAKA


KUTOKANA na kuchakaa haraka kwa noti ya shilingi 500 na kiwango chake kudumu kwenye mzunguko kwa miezi sita tu, Benki Kuu ya Tanzania (BoT), imesema inatarajia kubadili noti hiyo na kuwa ya sarafu.

Akizungumza na gazeti la Tanzania Daima juzi  kwenye viwanja vya maonesho ya kimataifa ya biashara, jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Kitengo cha Fedha, Abdul Dollah, alisema mabadiliko hayo yatafanyika hivi karibuni na sarafu hiyo itadumu kwenye mzunguuko kwa zaidi ya miaka 20 huku ikiwa na ubora wake.

Dollah alitaja sababu nyingine ya uchakavu huo ni kutokana na noti hiyo kushikwa na watu wengi kwenye mzunguko huku baadhi yao wakishindwa kuzihifadhi vizuri: 


“Tofauti na noti nyingine kama vile zile za sh 5,000 na 10,000 hizi utakuta mara nyingi uchakavu wake si kama ule wa sh 500 kwa sababu noti hizi watumiaji wake wengi ni wale wenye akaunti benki.”

No comments:

Post a Comment